Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayay, Karia wajitosa Urais TFF

UCHAGUZI Pict

Muktasari:

  • Uamuzi wa Mayay unakuja siku moja tangu TFF kutangaza Juni 16 kuanza mchakato wa kuchukua fomu za nafasi ya urais na ujumbe wa kamati ya utendaji ambao unatarajiwa kufungwa kesho, Ijumaa kwa kila mmoja kurudisha kabla ya saa 10 jioni.

NYOTA wa zamani wa Yanga, Ally Mayay amethibitisha kuingia kwenye mbio za kugombea urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ikiwa ni siku mbili baada ya kuchukua fomu ikielezwa ni mmoja wa wagombea wanne waliojitokeza hadi sasa.

Uamuzi wa Mayay unakuja siku moja tangu TFF kutangaza Juni 16 kuanza mchakato wa kuchukua fomu za nafasi ya urais na ujumbe wa kamati ya utendaji ambao unatarajiwa kufungwa kesho, Ijumaa kwa kila mmoja kurudisha kabla ya saa 10 jioni.

Akiwa katika msiba wa kumpoteza baba yake, Mayay alichukuliwa fomu na mchezaji mwenzake wa zamani, Amri Kiemba. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Mayay alithibitisha jambo hilo.

“Ndio, ni kweli nimechukua fomu na aliyenichukulia ni Kiemba kwa sababu nilikuwa kwenye mazingira magumu ya msiba wa baba yangu. Hata hivyo, nia na dhamira yangu ya kushiriki katika mchakato huu iko palepale,” alisema.

Kiemba ambaye alimwakilisha, alisema Mayay ambaye hii ni mara yake ya pili, anaamini ana mchango mkubwa wa kutoa kuendeleza mchezo wa soka kupitia uongozi.

“Ni haki ya kila Mtanzania kuchangia maendeleo ya nchi yake kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uongozi. Ally Mayay anaamini muda umefika kuwa sehemu ya uamuzi mkubwa kuhusu mustakabali wa soka letu,” alisema.

Mayay ni miongoni mwa wanasoka wachache waliowahi kucheza kwa kiwango cha juu nchini na baadaye kujikita katika uongozi, uchambuzi na maendeleo ya michezo. Mbali na Mayay, rais wa sasa wa TFF, Wallace Karia amechukua fomu ya kuwania muhula mwingine. Hadi jana jioni, wagombea wanne walikuwa wameshachukua fomu za kuwania urais, ingawa majina ya wawili wengine Mwanaspoti halikufanikiwa kuyapata.

Vyanzo vya karibu na mchakato huo vinaeleza kuwa baadhi ya wagombea wana historia kubwa katika usimamizi wa soka nchini, huku wengine wakihusishwa na klabu maarufu na vyama vya soka vya mikoa.

Uchaguzi wa TFF mwaka huu unatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na kuibuka kwa wagombea waliobobea katika nyanja mbalimbali. Nafasi nyingine zinazowaniwa katika uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 16 jijini Tanga ni wajumbe sita wa kamati ya utendaji ambayo hata hivyo, bado haijafahamika waliokuwa wamejitokeza hadi gazeti hili linakwenda mitamboni.