Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayanga atajwa AFC Leopard

Nairobi.  Jina la Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania, Salum Mayanga, limetajwa katika majina manne ya makocha wanaotakiwa na AFC Leopards inayoshiriki Ligi Kuu Kenya.

Katika majina hayo manne, linatakiwa lipatikane jina moja baada ya mchujo kisha atapewa kazi ya kuwanoa, mabingwa hao mara 13 wa Ligi Kuu Kenya, AFC Leopards juma lijalo baada ya kutangazwa.

Dennis Kitambi, ambaye nI kocha wa sasa, ataondoka Mei 8 kuelekea nchini Bangladesh kujiunga na kocha Stewart Hall kama kocha msaidizi katika klabu ya Saif SC ya Ligi Kuu ya nchini humo.

Katibu Mkuu wa timu hiyo, Oscar Igaida alisema wamepokea majina manne mpaka hivi sasa ambayo yanataka kurithi mikoba ya kocha Denis Kitambi.

“Tuko na majina manne ya makocha ambao mmoja wao atatajwa kocha mkuu juma lijalo lakini ataanza kazi Mei atakapoondoka Kitambi,” alisema katibu wa Ingwe,Oscar Igaida bila kutaja majina yao.

Hata hivyo Mwanaspoti linafahamu, kocha wa timu ya Taifa Tanzania, Salum Mayanga, Mfaransa Didier Gomes da Rosa na Rodolfo Zapata raia wa Argentina ni miongoni mwao wanaowania nafasi hiyo.

Gomes (48) kwa sasa anaifundisha klabu ya Ethiopia Coffee ya Ligi Kuu ya Uhabeshi na ameshinda Ligi Luu nchini Rwanda pamoja na Cameroon akiwa na vilabu vya Rayon Sport na Coton Sport.

Naye Zapata (51) amefanya kazi nchini Afrika Kusini, Nigeria na Gabon.

Hata hivyo, kocha Kitambi kutoka Tanzania, amefichua sababu zilizomfanya kukataa ofa ya kuendelea kukifundisha kikosi hicho.

“Ni kweli walinipa ofa nzuri lakini kwangu pesa si muhimu kama heshima ninayoenda kupata kule Asia,  Hall ni mlezi wangu, yeye ndiye aliyenilea nilipotemwa Ndanda FC hadi nilipo sasa,” alisema.

Kitambi aliongeza Hall alimpigania aingie Leopards Novemba 2016 kama msaidizi wake na sasa amepata kazi Bangladesh amemuhitaji tena, lakini pia anataka kusoma kozi ya ukocha ya UEFA baada ya kupata leseni ya CAF “A”,hivyo anaamini akiwa karibu naye sababu pia yeye ni mwalimu basi atapata darasa zuri.

Dennis Kitambi,  anaondoka Mei nane kuelekea nchini Bangladesh kujiunga na mwalimu wake Stewart Hall kama kocha msaidizi katika klabu ya Saif SC ya Ligi Kuu ya nchini humo.