Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maximo: Nyota wanne Simba kiboko

Emmanuel Okwi wa Simba (juu) akikabwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro wa Yanga.

Muktasari:

  • Maximo alisema baada ya kugundua Simba inazuia, alitumia mifumo mitatu tofauti ya 4-4-2, 4-2-3-1 na 4-3-3, lakini mabeki wanne wa Simba waliokuwa kwenye mstari wa mwisho wakiongozwa na Joseph Owino raia wa Uganda, walikuwa hawatoki eneo lao.

HASIRA za Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo, sasa ni kwa Stand United atakayokutana nayo Jumamosi, lakini amedai  kwamba Simba walipaki basi ndio maana ikawawia vigumu kushinda juzi Jumamosi.

Maximo alisema baada ya kugundua Simba inazuia, alitumia mifumo mitatu tofauti ya 4-4-2, 4-2-3-1 na 4-3-3, lakini mabeki wanne wa Simba waliokuwa kwenye mstari wa mwisho wakiongozwa na Joseph Owino raia wa Uganda, walikuwa hawatoki eneo lao.

Pia alisema walikuwa makini kwa kucheza mtu na mtu wakiwanyima kabisa nafasi ya kucheza wachezaji wake.

 Akizungumza na Mwanaspoti, Maximo alisema: “Simba walikuwa wanazuia, mabeki wao wanne wa nyuma walikuwa hawatoki eneo lao hivyo kukawa hakuna nafasi ya kupenya langoni mwao. Na walipokuwa wanashambulia, walikuwa wanacheza mipira mirefu langoni mwetu kwa kushtukiza, lakini kwenye eneo lao lilibaki hivyo hivyo hali ambayo ilinilazimu kubadilisha mifumo mitatu tofauti, nilitumia 4-4-2, 4-2-3-1 na 4-3-3 ambayo nayo haikutusaidia.”

Katika mfumo wa 4-4-2, aliwachezesha mabeki wanne nyuma wakati Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ walicheza kati, kulia Juma Abdul na kushoto Oscar Joshua, viungo wanne waliocheza ni Mnyarwanda Mbuyu Twite kuzuia, Hassan Dilunga kushambulia, Mbrazili Andrey Coutinho winga ya kushoto na kulia  Mrisho Ngassa na wawili walicheza straika mbele, Mbrazili Genilson Santos ‘Jaja’ na Mnyarwanda Haruna Niyonzima ‘Fabregas’ alicheza nyuma yake kwa staili ya kuzunguka eneo lote la mbele.

Alipoingia Simon Msuva kuchukua nafasi ya Niyonzima, aliwachezesha 4-2-3-1 ambapo nyuma wakiwa kama kawaida, Yondani na Cannavaro, watatu waliocheza kati ni Coutinho, Ngassa na Msuva wakati Jaja aliachwa mbele.

Baadaye alimaliza na 4-3-3 baada ya Hamis Kiiza raia wa Uganda kuingia na Salum Telela kuchukua nafasi ya Juma Abdul ambaye alitoka baada ya kubanwa na misuli.

Nyuma aliongezeka Telela peke yake, kati walicheza Mbuyu, Dilunga na Msuva na mbele kulikuwa na Coutinho, Kiiza na Ngassa.  

Maximo aliongeza kuwa, alifanya mabadiliko yote lakini walioingia kwa timu ya  Simba nao walikuwa vizuri.

“Kwa ujumla nawapongeza Simba hasa beki ilifanya vizuri ndiyo maana, tulimaliza kwa suluhu,” alisema.