Mastaa Yanga wachekelea...

NYOTA wa Yanga sasa wamepata ganda la ndizi, hivyo ndio unaweza kusema baada ya ujio wa kocha Cedrick Kaze wamepata nafuu ya usaidizi wa lugha.

Kaze sasa ni kama amepewa kazi ya kuwatafsilia wachezaji lugha ya kifaransa ambayo imezoeleka kutumiwa na kocha wao mkuu Nasreddine Nabi.

Leo katika mkutano na waandishi wa habari Nabi kama kawaida yake alitumia lugha ya kifaransa na kocha wake msaidizi Kaze ndiye aliyekuwa akitafsili lugha hiyo.

Awali Nabi alikuwa anamtumia kijana anayefahamika kwa jina la Karim lakini kwenye mkutano wa leo haikuwa hivyo, ukiachana na kwenye mikutano pia itakuwa rahisi kwa wachezaji uwanjani itakuwa rahisi kumtumia Kaze.

Ujio wa kocha huyo ni ahuheni kwa wachezaji kwani atakuwa msaada kwao pale watakaposhindwa kuelewa kile wanachoelekezwa na kocha mkuu.