Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa waliotikisa Afrika kwa ubora wao

Muktasari:

  • Hivi sasa Ulaya yote ni Mohamed Salah, Sadio Mane wa Liverpool, Pierre-Emerick Aubameyang na Alex Iwobi wa Arsenal ambao wanatamba hawa walifanya makubwa kwa kipindi kirefu na kugeuka mifano kwa vijana wanaochipukia kwenye soka.
  • Mastaa 10 waliotisha na kuacha sifa Ulaya na Afrika.

Dar es Salaam.Unapozungumzia soka ya Afrika, utakuwa hujatenda haki endapo utawaacha baadhi ya wachezaji waliotisha katika medani ya soka Afrika.

Kuna nyota kadhaa ambao enzi zao walifanya makubwa kwenye Ligi mbalimbali  barani Ulaya na timu zao za taifa. Waliitendea haki soka yao walipokuwa Ulaya na hata walipotumikia mataifa yao ya Afrika.

Hivi sasa Ulaya yote ni Mohamed Salah, Sadio Mane wa Liverpool, Pierre-Emerick Aubameyang na Alex Iwobi wa Arsenal ambao wanatamba hawa walifanya makubwa kwa kipindi kirefu na kugeuka mifano kwa vijana wanaochipukia kwenye soka.

Mastaa 10 waliotisha na kuacha sifa Ulaya na Afrika.

George Opong Weah

Kwa sasa ni Rais nchini kwao Liberia na mara kadhaa amekuwa akikumbushia kucheza soka huku pia akisaidia kutengeneza nafasi za vijana wanaocheza soka nchini kwake.

Alizaliwa 1966 na alianza maisha yake ya soka akiwa na miaka 15. Miaka saba baadaye alichaguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Liberia.

Kama ilivyo kwa wachezaji wenzake kutoka Afrika Magharibi, nyota huyo akatoka nchini kwao Liberia na kujiunga na soka la Ufaransa ambapo huko alifanikiwa kushinda mataji mbalimbali akiwa Ufaransa.

Mwaka 1993 alijiunga na PSG na kutwaa Kombe la Ufaransa na ubingwa wa Ligue 1.

Akashinda tuzo ya Mchezaji Bora Afrika pamoja na Tuzo ya mchezaji Bora Ulaya lakini kubwa zaidi akichaguliwa kushinda uchezaji bora wa mwaka wa Fifa.

Mara baada ya kuachana na PSG alijiunga na klabu za Al Jazira, Marseille, Chelsea, AC Milan na Manchester City.

Jay Jay Okocha

Okocha alikuwa maarufu kwa ‘vyenga’. Alikupiga chenga na kisha anakucheza, ilikuwa staili yake wakati mwingine. Aliwahi kutwaa Tuzo ya mchezaji Bora Nigeria mwaka 1995, 1997, 2000, 2002, 2003, 2004 na 2005. Jina lake hasa ni Augustine Azuka Okocha lakini wengi wanamtambua kama Jay Jay Okocha.

Ukiachana na makubwa aliyoyafanya kwenye klabu alizozichezea, nyota huyo alifanya pia makubwa akiwa na timu ya taifa ya Nigeria akishiriki vyema kwenye michuano kadhaa ikiwemo Kombe la Dunia mwaka 1994 na mwaka 1998, Michezo ya Olimpiki mwaka 1996 pamoja na Fainali za Afrika ( Afcon).

Rashidi Yekini

Nyota mwengine raia wa Nigeria ambaye kwa sasa ni marehemu. Rashid Yekini alizaliwa mwaka 1963 na kufariki mwaka 2012.

Anatajwa kama mchezaji bora wa muda wote nchini Nigeria akifunga goli la kwanza la timu yake ya taifa ya Nigeria kwenye Fainali za Kombe la Dunia. Alizichezea kwa mafanikio klabu Shooting Stars na Vitoria Setubal za Nigeria lakini pia akifanya vizuri akiwa na timu yake ya taifa mpaka akachaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka barani Afrika akishinda tuzo hiyo kwa miaka miwili mfululizo, yaani mwaka 1993 na mwaka 1994.

Samuel Eto’o

Nyota wa kikosi cha Cameroon aliyewahi kufanya makubwa kwenye soka la kimataifa akitamba na klabu kadhaa ikiwemo Inter Milan, Barcelona na Chelsea. Alishinda pia mara nne tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Afrika.

Samuel Eto’o, nyota aliyetamba kwenye nafasi ya ushambuliaji, akishinda mataji kadhaa akiwa na timu yake ya taifa ambapo aliwai kuiongoza Cameroon kushinda michuano ya Afrika na kushinda mataji mawili huku kwenye Olimpiki timu yake ikishinda medali ya dhahabu mwaka 2000 Sydney.

Didier Drogba

Ametengeneza heshima kubwa katika ulimwengu wa soka akishinda mataji na kufanya mengi katika soka.

Ni mmoja kati ya wachezaji waliofanya vizuri wakiwa na kocha Jose Mourinho  pale Stamford Bridge ambako katika mataji matatu ya Ligi Kuu ambayo kocha huyo ameyashinda akiwa na Chelsea, Didier Drogba amekuwa kama mhimili huku akiongeza na Ligi Kuu moja akiwa chini ya kocha Carlo Ancellotti. Akiwa na timu ya taifa ya Ivory Coast aliiongoza katika michezo 104 na kufunga magoli 65 na hadi sasa, anashikilia rekodi ya mchezaji mwenye magoli mengi kwa muda wote timu ya taifa.

Nwankwo Kanu

Mnigeria Nwankwo Kanu alizaliwa 1976 na amekuwa miongoni mwa wachezaji wa taifa lake ambao wamecheza michezo mingi ya kimataifa akiwa na klabu kadhaa kubwa barani kama vile Ajax Amsterdam, Arsenal FC, Portsmouth FH, West Brom  na FC Heartland.

Kanu ni mshindi wa mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, pia anamedali ya Olympics na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hossam Hassan Hussein

Mwaka 1966 katika nchi ya Misri alizaliwa gwiji huyu ambaye mpaka leo ameacha alama katika kikosi chake cha timu ya taifa akiwa mfungaji bora wa kipindi chote katika timu hiyo akifunga magoli 70 katika michezo 169 aliyoichezea timu ya Misri akiwa mshambuliaji.

Anakumbukwa vyema akicheza kwa muda mrefu sambamba na pacha wake ambaye mara nyingi walikuwa wakicheza klabu moja, yani ilikuwa kawaida ukimsajili mmoja basi unamsajili na pacha wake. Hossam alichezea Al Ahly aki vunja rekodi nyingi. Lakini pia akizichezea klabu kadhaa za nchini Switzerland na Ugiriki.

Aliwahi kuwa mfungaji bora wa Afcon mwaka 1998 na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.

 Yaya Toure

Yaya Toure alizaliwa mwaka 1983 huku akifanya makubwa kwenye soka mpaka kubatizwa jina la Treni Binadamu kutokana na uwezo wake na kasi yake akiwa uwanjani akitumia vizuri misuli yake iliyotengenezwa kwa umbo lake na mazoezi mengi.

Anakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya akiwa na klabu ya Manchester City licha ya sasa kuichezea klabu ya Olympiacos.

Alistaafu kucheza soka la kitaifa akiwa ana miaka 32 lakini alirejea tena kwenye timu ya taifa miaka miwili baadae mara baada ya kutangaza kuengua maneno yake ambapo alitangaza hivyo ili kuisaidia timu yake ya Ivory Coast iweze kupambana na kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 lakini hakufanikiwa.

Roger Milla

Albert Roger Mooh Miller ndilo jina lake kamili lakini wengi wakimtambua kama Roger Milla alizaliwa mwaka 1952 na alikuwa moja kati ya wachezaji wachache wa mwanzoni waliocheza soka la kimataifa.

Alikuwa sehemu ya kikosi cha Cameroon kilichofanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia.

Alianza kucheza soka mwaka 1965 akiwa na klabu ya Eclair Club of Douala na akajiunga na klabu za Ufaransa.

Alizichezea klabu za Monaco na Bastia ambapo alishinda mfululizo mataji ya Kombe la Ufaransa mwaka 1980 na mwaka 1981.

Aliisaidia Cameroon kutwaa ubingwa Afcon mara mbili na alikuwa kwenye fainali za Kombe la Dunia 1990 na kuweka rekodi ya mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kufunga goli kwenye fainali hizo.

Abedi Ayew

Alizaliwa miaka 54 iliyopita   ni Pele wa Ghana. Aliitwa jina hilo kutokana na kufanana kwake  kiuchezaji na gwiji wa soka la Brazil, Pele. Ayew ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 1992/93 akiwa na  Marseille  na moja la Afcon katika miaka yake  16 ya timu yake ya taifa ambapo aliiongoza kama nahodha kwa miaka sita kabla ya kustaafu 1998.