Mastaa wa kike wanavyopenda soka kisa watoto wao

MADONNA ni shabiki mkubwa wa Benfica kwa sasa, kisa mtoto wake David Banda anachezea timu hiyo.
Mwimbaji huyo maarufu wa Pop, Madonna amekuwa akionekana mara kadhaa huko Estadio da Luz akiwa na mwanaye David kutazama kikosi cha kwanza cha Benfica kikicheza huku akiwa na matumaini kibao, siku moja mtoto wake naye atacheza kwenye kikosi hicho cha wakubwa. Kutokana na hilo, Madonna amekuwa akitumia muda mwingi sana huko Ureno tangu mwanaye huyo aliposajiliwa kwenye akademia ya Benfica.
Madonna, ambaye aliwahi kutamba na wimbo wake wa ‘Material Girl’ amekuwa akipiga picha na kuzishea kwenye mitandao ya kijamii kuonyesha mwanaye anafanya mazoezi na alifurahi sana siku ambayo mtoto wake alishinda huko mazoezini.
Hata hivyo, Madonna si mwanamke wa kwanza maarufu, ambaye amejikuta akipenda soka kwa sababu tu mwanaye amekuwa akijihusisha na mchezo huo kwa kuucheza akiwamo mrembo Anna Paquin, mwigiaji wa New Zealand.
Victoria Beckham
Mwimbaji huyo wa zamani wa kundi la muziki wa Pop la Spice Girls, mrembo Victoria amekuwa hakauki kwenye mazoezi ya mpira wa miguu kuwatazama watoto wake na kiume Brooklyn, Romeo na Cruz. Mumewe pia, ambaye aliwahi kucheza kwenye timu maarufu kama Manchester United na Real Madrid amekuwa bega kwa bega katika kumpa nafasi mkewe kuwasapoti watoto wao wanaopenda soka. Victoria ametoa nafasi kwa watoto wake kufuata nyayo za baba yake, kucheza soka.
Britney Spears
Staa mwingine wa muziki wa Pop. Britney Spears ameamua kutumia muda wake wa kuachana na utunzi wa nyimbo na kuamua kuwapeleka watoto wake Jayden James na Sean Preston Federline kwenye mchezo waupendao, soka. Mwanzoni Britney alipata shida sana alipokuwa akiwapeleka watoto wake mazoezini kutokana na umaarufu wake, lakini jambo hilo halikumkatisha tamaa na muda wote alihakikisha watoto wake wanafurahia kufanya kitu wanachokipenda. Kwa kuwatazama watoto wake, Britney amejikuta akiwa mpenzi mkubwa wa mchezo wa soka.
Madonna
Mtoto wa gwiji huyo wa muziki, David Banda kwa sasa amesainiwa kwenye akadamia ya Benfica huko Ureno. Kila zinapofika wikiendi, Madonna amekuwa hakauki kwenda kumshangilia mtoto wake huyo anapokuwa kwenye mechi au mazoezi. Wawili hao, mama na mtoto pia mara kadhaa wamekuwa wakihudhuria mechi za kikosi kikubwa cha Benfica ikiwa ni sehemu ya kumsaidia mwanaye kuwa na uchu wa siku moja kuichezea timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Ureno na michuano mingine mingi ya Ulaya. Ilielezwa supastaa Cristiano Ronaldo aliripotiwa kumpigia simu Modonna baada ya kusikia David anakwenda kujiunga na Benfica na kumtaka apelekwe Sporting Lisbon, alikotokea staa huyo wa Real Madrid.
Kate Winslet
Huko Hollywood, mwigizaji mrembo Kate Winslet ameonekana mara kadhaa akimchukua mwanaye, Joe na kumpeleka kucheza soka na akiwa na umri wa miaka 14, mtoto huyo anaonekana kuwa kwenye hali nzuri inayompa nafasi ya kupasua na kufikia soka la kulipwa. Joe ni mtoto aliyetokana na uhusiano wa kimapenzi baina ya mrembo Kate na Sam Mendes na wazazi hao mara kadhaa wameonekana kwenda kumshangilia mtoto wao kwa pamoja akicheza. Jambo hilo limedaiwa kumfanya Joe kuwa na juhudi na jitihada za kuja kuwa staa mkubwa kwenye soka la dunia.
Jennifer Garner
Mrembo huyo mwigizaji maarufu ameonekana akiwasimamia watoto wake kuhakikisha wanacheza soka bila hata ya sapoti ya baba yao, Ben Affleck. Mama huyo, Jennifer ameonekana akifanya kwa furaha yote kitendo cha kuwachukua watoto wake, Violet, Samuel na Seraphina kwenda kufanya mazoezini na kumekuwa na imani kubwa wanaweza kufikia kiwango kikubwa cha soka la uwanjani.
Uwezo wa watoto hao ndicho kitu kinachomfanya mrembo Jennifer kuweka juhudi za kuwapeleka mazoezini. Jennifer aliwahi kuolewa na Ben Affleck, ambaye pia aliwahi kumuoa mwimbaji Jennifer Lopez.
Hedi Klum
Mrembo Heidi Klum ni staa mwingine wa kike mwenye jina kubwa kwenye sanaa, ambaye amekuwa na jitihada za kuwapeleka watoto wake kufanya mazoezi ya soka. Mwanamitindo huyo, ana watoto wawili aliowapata kwenye ndoa yake na Seal na mmoja kwenye uhusiano wake na dereva wa Formula One, Flavio Briatore, amekuwa na jitihada za kuhakikisha watoto wake wote wanajihusisha na soka na kuucheza mchezo huo kwa ufasaha zaidi.
Mtoto wa watoto wake, mrembo Heidi Klum ni wa kike, Leni Samuel na amekuwa hodari kweli kweli kwenye kuucheza mpira wa miguu.
Reese Witherspoon
Mshindi wa tuzo ya Oscar na ameweka umaarufu wake kando na kuhakikisha anasimamia kwa kiwango chote kumfanya mtoto wake wa kiume, Deacon anafikia mafanikio makubwa kwenye soka.