Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa BDL walivyoiteka Taifa Cup

Muktasari:

  • Wachezaji hao ni Haji Mbegu, Ally Faraji (Dar City) walioichezea Unguja na Mwalimu Heri pamoja Evance Davies (Outsiders) walioichezea timu ya Mkoa wa Kigoma.

BAADHI ya wachezaji wanaocheza katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) waliocheza katika mikoa mbalimbali kwenye mashindano ya kombe la taifa mjini Dodoma walikuwa kivutio kutokana na kuonyesha ubora.

Wachezaji hao ni Haji Mbegu, Ally Faraji (Dar City) walioichezea Unguja na Mwalimu Heri pamoja Evance Davies (Outsiders) walioichezea timu ya Mkoa wa Kigoma.

Wengine ni Amin Mkosa na Jordan Jordan (Mchenga Star) walioichezea Kigoma, Fotius Ngaiza (Vijana ‘City Bulls’) aliyechezea Dodoma na Stanley Mtunguja wa Ukonga Kings aliyekipiga akiwa amevaa jezi ya Kigoma.

Kwa upande wanawake, Noela Renatus, Tumaini Ndossi na Bhoke (Vijana Queens) waliichezea Unguja huku Tumwagile Joshua na Jesca Lenga wanaokipiga DB Troncatii walichezea timu ya Mkoa wa Mara.