Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masoud na Dodoma Jiji ni jambo la muda TU

MUDA wowote kuanza sasa uongozi wa Dodoma Jiji utatangaza kuachana na benchi lake la ufundi linaloongozwa na kocha mkuu, Mbwana Makata kubwa lililosababisha hilo ni mwenendo mbaya wa matokeo.
Mwanaspoti limepata taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho na kujilizisha uongozi baada ya kukubaliana kuachana na Makata pamoja na wasaidizi wake nafasi hiyo itachukuliwa na Mrundi Masoud Djuma.
Djuma aliyewahi kuifundisha Simba 2017, leo jioni atawasili nchini kutokea Burundi kisha kesho saa 4:00 asubuhi atakula tena mwewe kwenda Dodoma kumalizana na waajiri wake hao wapya.

Uongozi wa Dodoma umekubaliana kumpatia Djuma mkataba wa miezi sita kukinoa kikosi hicho mpaka mwisho wa msimu na ndani yake kuna kipengele cha kuongeza mwaka mmoja kama watalizia utendaji wake wa kazi.

"Kuna majina ya makocha watano wapya ambayo yamependekezwa kwa uongozi wa juu na wao ndio watafanya maamuzi ya yupi ambaye atakuja kuifundisha timu yetu," amesema Katibu wa timu hiyo ya Dodoma, Fortunatus Johnson.