Maskini Neymar kuikosa Man United

Muktasari:

 

  • Neymar kutokana na hali yake atakuwa nje ya uwanja kwa wiki 10 kuuguza jeraha lake

Paris, Ufaransa. Neymar atakosa mechi zote mbili za Ligi ya Mabingwa kati ya Paris Saint-Germain dhidi ya Manchester United baada ya mabingwa hao wa Ufaransa kuthibisha kuwa nyota huyo atakuwa nje ya uwanja wa wiki 10 kuuguza majeraha yake.

Hata hivyo, Neymar hatofanyiwa upasuaji, PSG imesema Brazili huyo atapewa matatibu yatakayomwezesha anarudi kwa wakati katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Aprili kama watafanikiwa kufuzu.

"Baada ya majadiliano ya wataalum tumefikia makubaliano ya Neymar kupewa matibabu ya kawaida kutibu jereha lake," ilisema klabu hiyo.

Neymar aliumia wakati wa mchezo wa Komba la Ufaransa kati ya PSG dhidi ya Strasbourg wiki iliyopita, jambo lililomfanya kocha Thomas Tuchel kuondoa nyota huyo katika kikosi chake kitakachocheza na Man United kwenye Uwanja Old Trafford hapo Februari 12.

Mechi ya marudiano itachezwa Machi 6, lakini muda uliotangazwa atarudi na klabu yake utakuwa ni mechi za robo fainali Aprili 9 na 10. Mechi za marudiano zitafanyika wiki inayofuata.