Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa, Mgunda ni suala la muda tu

MGUNDA Pict

Muktasari:

  • Vita ilimtaka Mgunda kwenda kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji, ambako straika huyo ni mmoja wa mastaa waliotakiwa na aliyekuwa kocha Youssouf Dabo aliyewahi kuifundisha Azam FC.

MASHUJAA haijamkatia tamaa aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Ismail Mgunda aliyekuwa ametimkia AS Vita ya DR Congo katika dirisha dogo msimu huu kabla ya kurejea nchini hivi karibuni.

Vita ilimtaka Mgunda kwenda kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji, ambako straika huyo ni mmoja wa mastaa waliotakiwa na aliyekuwa kocha Youssouf Dabo aliyewahi kuifundisha Azam FC.

Mgunda ambaye msimu huu ameifungia Mashujaa mabao mawili, alichukuliwa na Dabo, lakini hakufanikiwa kuendelea kucheza baada ya kocha huyo kuondoka.

Taarifa za ndani kutoka AS Vita zililiambia Mwanaspoti, Mgunda ameondolewa kutokana na kiwango chake kuonekana kiko chini.

“Mabosi walimuondoa baada ya kocha aliyewaleta kuondoka, wangebaki kama angekuwa bora ila kwa ukubwa wa timu waliona hawawezi kuendelea naye.”

Taarifa kutoka Mashujaa zinasema; “Mgunda amerejea tumesikitika kuona amekuwa kule kwa muda mfupi, lakini kwetu bado ni mchezaji wetu bora na alikuwa anatusaidia sana, aliondoka kwa sababu ya kimaendeleo.

“Tumepanga kumtafuta aje tuongee naye kwa kina ili kama atakubaliana na sisi arudi klabuni kwake kuendelea na pale alipoishia, unajua alikuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza kama atakubali tutakuwa naye kwa msimu ujao.”

Mashujaa inashika nafasi ya nane katika ligi ikiwa imecheza mechi 28, imeshinda nane, sare tisa na kupoteza 11, huku ikisalia na mechi mbili kumaliza mzunguko wa pili wa msimu. Timu zinapigania kutocheza playoffs.