Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI yumo dhidi ya FC Porto leo usiku mchezo wa kirafiki

Muktasari:

  • Aziz KI aliyetua Wydad hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga, wakati kikosi hicho kinapoteza mbele ya Sevilla kwa bao 1-0, Mei 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mohammed V uliopo Morocco, alikuwa jukwaani.

BAADA ya kuukosa mchezo wa kwanza wa kirafiki ambao Wydad Athletic Club ilicheza dhidi ya Sevilla, hatimaye leo Mei 31, 2025 kiungo mshambuliaji, Stephane Aziz KI amejumuishwa kwenye kikosi kitakachoikabili FC Porto ya Ureno.

Aziz KI aliyetua Wydad hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Yanga, wakati kikosi hicho kinapoteza mbele ya Sevilla kwa bao 1-0, Mei 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mohammed V uliopo Morocco, alikuwa jukwaani.

Taarifa iliyotolewa na Wydad leo Jumamosi kabla ya kukabiliana na FC Porto majira ya saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mohammed V, Aziz KI atakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo huo wa pili wa kirafiki.

Katika kikosi hicho chenye wachezaji 25 ambacho ndicho kitakwenda kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani, pia yupo mshambuliaji Mtanzania, Seleman Mwalimu.

Mwalimu maarufu Gomez aliyetua Wydad Januari mwaka huu akitokea Singida Black Stars, alicheza mechi iliyopita dhidi ya Sevilla akiingia dakika ya 80.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni Omar Aqzdaou, Youssef El Motie, El Mehdi Benabid, Fahd Moufi, Ayoub Boucheta, Ayman Dairani, Abdelmounaim Boutouil, Jamal Harkass, Mohammed El Jadidi, Mohamed Moufid, Zouhair El Moutaraji, Oussama Zemraoui, El Mehdi El Moubarik, Zakaria Fathi, Thembinkosi Lorch, Stephane Aziz KI, Ismael Benktib, Mohamed Rayhi, Samuel Obeng, Seleman Mwalimu, Cassius Mailula, Zakaria Nassik, Nordin Amrabat, Mickael Malsa na Hamza Hannouri.

Kwa sasa Wydad ipo kwenye maandalizi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia la Klabu nchini Marekani itakayoanza Juni 14 hadi Julai 13, 2025 ikishirikisha timu 32, huku timu hiyo ikipangwa Kundi G na Manchester City (England), Juventus (Italia) na Al Ain (UAE).