Mashabiki Yanga waipamba Airport

Muktasari:
- Mashabiki wa Yanga wametinga uwanjani hapo wakiisubiri timu yao ikitokea Zanzibar baada ya jana Jumapili kutwaa taji la FA kwakuifuga Singida Black Stars mabao 2-0, mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan, Zanzibar na leo wanarejea wakiwa na taji hilo.
LICHA ya mashabiki kuzuiliwa kuingia ndani ya eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, eneo la nje ya uwanja huo limefunikwa na rangi ya kijani, nyeusi na njano.
Mashabiki wa Yanga wametinga uwanjani hapo wakiisubiri timu yao ikitokea Zanzibar baada ya jana Jumapili kutwaa taji la FA kwakuifuga Singida Black Stars mabao 2-0, mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan, Zanzibar na leo wanarejea wakiwa na taji hilo.
Ili kunogesha sherehe yao ya kutwaa taji lao la tano msimu huu , Yanga itafanya sherehe ya kuzungusha mataji yao wakiwa na gari ya wazi ambalo tayari limewasili ikisubiri wachezaji watoke.
Yanga huenda ikafanya kile walichokifanya msimu uliopita kwa kusimamisha shughuli nyingi ikilipitisha Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Bara baadhi ya maeneo ikikusanya maelfu ya mashabiki wa timu hiyo ambapo kwa ratiba iliyotolewa na klabu hiyo shughili za ubingwa zitaanzia Airport, Tazara, Keko, Karume, Msimbazi na hatimaye makao makuu ya klabu hiyo Jangwani.
Msimu huu Yanga wametwaa taji la Toyota Cap, Ngao ya Jamii, Mapinduzi Cap, Kombe la Shirikosho la Azam na Ligi kuu bara likiwa ni taji lao la 31.