Mashabiki waziwahi City na Simba, Mwanaspoti yakata kiu

Monday January 17 2022
Mashabiki PIC
By Saddam Sadick

Mbeya. Wakati wadau wakisubiri kwa hamu mchezo baina ya Mbeya City na Simba, tayari baadhi ya mashabiki wameshawasili Uwanjani kushuhudia kandanda hiyo.

Mchezo huo unatarajia kupigwa saa 10:00 jioni katika uwanja wa Sokoine jijini hapa ukiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu raundi ya 12 kwa Mbeya City na 11 kwa Wekundu.

Tofauti na siku za nyuma mashabiki kupanga foleni, leo imekuwa tofauti kwani leo hakuna utaratibu huo kutokana na milango kufunguliwa mapema na kuzama uwanjani.

Pia kiingilio katika mchezo huo ni Sh 5,000 bila kujali Jukwaa Kuu au mzunguko jambo ambalo limefanya kutokuwepo changamoto yoyote.

Pamoja na mashabiki hao kuwahi uwanjani, lakini hawakuwa mbali na gazeti lao pendwa, Mwanaspoti, huku wakiendelea kuperuzi wakisubiri muda wa mpambano huo

Advertisement