Mashabiki wasuasua Sokoine

Tuesday September 28 2021
sokoine pic
By Saddam Sadick

Mbeya. Zikiwa zimebaki dakika chache kuanza kwa mchezo wa Ligi Kuu kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons, lakini hali na mwitikio wa mashabiki uwanjani imekuwa si ya kuridhisha.

Hadi sasa ni dakika 30 pekee zimebaki kufikia saa 10:00 jioni ambapo mechi hiyo inatarajiwa kupigwa katika dimba la Sokoine jijini hapa ukiwa wa kwanza katika Ligi Kuu msimu huu wa 2021/22.

Tayari timu zote zimeshaingia uwanjani zikiendelea kupasha misuli tayari kwa mchezo huo na kusaka pointi tatu za kwanza katika Ligi hiyo kubwa hapa nchini.

Katika majukwaa ya mashabiki bado namba ni ndogo sana na muitikio wa kuingia kushuhudia mechi hiyo ni mdogo licha ya milango kufunguliwa mapema.

Kada zinazoonekana ni askali Polisi na kundi la wapiga ngoma wa Mbeya City pamoja na viongozi wa soka na timu ambao wamekaa jukwaa Kuu sambamba na waandishi wa habari.

Advertisement