Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki, Simba, Yanga kuliamsha Kizimkazi Festival

KIZIMKAZI Pict

Muktasari:

  • Tamasha hilo litafanyika Mkoa wa Kusini na litfunguliwa na Rais Samia kwenye Uwanja Mpya wa Suluhu Academy.

WAKATI Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Kizimkazi litakalofanyika kwa siku nane kuanzia Julai 19, mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga watakiwasha kusaka mbabe baina yao ikiwa ni kunogesha tamasha hilo la mwaka 2025.

Tamasha hilo litafanyika Mkoa wa Kusini na litfunguliwa na Rais Samia kwenye Uwanja Mpya wa Suluhu Academy.

Mwenyekiti wa tamasha hilo, Mahfoudh Said Omar alisema mbali na Rais Samia, pia viongozi na wageni mbalimbali mashuhuri na maarufu kutoka ndani na nje ya nchi wataudhuria.

Alisema mbali na tamasha kuzindua miradi mbalimbali, litakuwa pia na burudani ya mechi ya mashabiki wa watani wa jadi, Simba na Yanga.

Vilevile itashindanisha wachezaji wa mbio za ngalawa, baiskeli, bao, karata na zuma.

Mbali na michezo hiyo, Omar alisema kutakuwa na mchuano mwingine wa taarabu asilia na bendi kongwe maarufu za dansi nchini za Msondo na Sikinde.

Pia wasanii wa Bongo Fleva, Rayvanny na Marioo watatumbuiza sanjari na makundi ya taarabu ya Modern Taarab ni Jahazi jicho kwa jicho na Zanzibar One Modern taarabu,".

Alisema kwa upande wa singeli mchuano utakuwa kati ya Dullah Makabila na Shollo Mwamba na kwamba maandalizi ya tamasha hilo lenye kauli mbiu ya  'Kizimkazi Kumenoga' yanakwenda vizuri.

Katibu Mkuu wa tamasha hilo, Ahmed Abdulhamid Hamis amesema miradi ya maendeleo inayofungamana na tamasha hilo itazinduliwa ndani ya siku hizo nane.

Alisema katika matukio ya tamasha hilo pia kutakuwa na kongamano la nishati safi ili kuungana na championi wa nishati safi Rais Samia.

Hamis amesema kabla ya tamasha hilo kuanza,   kutakuwa na mafunzo ya siku sita ya ujasiliamali kwa wavuvi, wasanii, watalii na walimu kuanzia Julai 12.

"Pia kutakuwa na dua maalumu ya kumuombea Rais wa Zanzibar,  Dk Hussein Mwinyi na Rais Samia  itakayofanyika Mnazi mmoja Zanzibar.

Muasisi wa Kazimkazi Festival, Said Hamad Ramadhan amesema tamasha  limekuwa kichocheo cha kuwa na maendeleo katika mkoa huo.

"Limeongeza fursa mbalimbali za biashara na hata watalii kuja,"  amesema Ramadhan.