Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu Zanzibar kufanyiwa maboresho

LIGI Pict

Muktasari:

  • Amesema, ili kupata udhamini wa uhakika na kukua kwa klabu za Zanzibar, wanahitaji kuwa na Ligi Kuu bora na yenye ushindani.

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Tabia Maulid Mwita, amesema wizara hiyo inashirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) kuiboresha Ligi Kuu ya ZPL kwa lengo la kupata wadhamini wengi na wa uhakika.

Amesema, ili kupata udhamini wa uhakika na kukua kwa klabu za Zanzibar, wanahitaji kuwa na Ligi Kuu bora na yenye ushindani.

Katika hilo, waziri huyo amesema hali hiyo ndio sababu Serikali ilifikia uamuzi wa kuitafutia udhamini na kupata Mdhamini Mkuu ambaye ni PBZ na Azam Media upande wa haki za matangazo.

Hayo ameyasema leo Jumanne Juni 17, 2025 wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Wingwi, Kombo Mwinyi Shehe katika mkutano wa Baraza la Wawakilishi.

Mwakilishi huyo amesema timu za Tanzania Bara ikiwemo Simba, Yanga na Azam zimepiga hatua kubwa katika mashindano mbalimbali ya ndani na ya kimataifa kutokana na ufadhili na uwezeshwaji mkubwa unaofanywa na matajiri na wadhamini ambao wamejikita kuwekeza kwenye michezo.

Hivyo, alitaka kufahamu kuwa Serikali ina mkakati upi wa kuzitafutia timu ufadhili na Serikali itaanza lini kufanya ‘lobbing’ kwa wawekezaji waliopo ndani na nje ya nchi kuzisaidia timu za Zanzibar.

Tabia amesema kwa kushirikiana na ZFF, ndiyo maana hivi sasa baadhi ya klabu zimeweza kupata udhamini.