Mashabiki Simba watii agizo la CAF

Saturday December 05 2020

AMRI ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuruhusu mashabiki nusu kuingia uwanjani kwenye michezo ya  Ligi ya Mabingwa imezingatiwa leo kwenye mchezo wa  marudiano kati ya Simba na Plateau United ya Nigeria.
Mashabiki wanaonekana kuwa sio wengi kuanzia nje na wale wa ndani ya uwanja ambao tayari wameingia na kuzishuhudia timu hizo zikipasha misuli ikiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo kuanza.

Caf imeruhusu mashabiki 30,000 tu kushuhudia mchezo huo licha ya uwezo wa uwanja wa Mkapa kubeba mashabiki 60,000 na Hali hiyo ni  imetokana na uwepo janga la Corona ambalo limezidi  kuitikisa Dunia.
Hata hivyo shangwe za mashabiki wa Simba sio kubwa licha ya mechi ya kwanza kushinda bao 1-0 Nigeria kupitia kwa Clatous Chama.

Ukiachana na hilo, awali mechi ilitarajiwa kuanza saa 11:00 jioni, lakini saa 11:11 wameanza kuingia wachezaji wa akiba wa timu zote mbili.
Huku vikosi vinavyoanza vimeingia 11:12 angalau kelele za Simba zikasikika kwa nguvu wakishangilia mastaa wao.

____________________________________________________________

Na Oliver Albert na Olipa Assa

Advertisement