Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marefa wa ngumi kupigwa msasa

NGUMI Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa TPBRC, Emmanuel Saleh alipokuwa anafunga kozi ya mafunzo kwa waamuzi yaliyofanyika jana Fit Poa Gym iliyopo Masaki, Dar es Salaam.

KAMISHENI ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imesema itaendelea kutoa kozi ya waamuzi wa mchezo ili kuongeza weledi katika kazi zao.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mwenyekiti wa TPBRC, Emmanuel Saleh alipokuwa anafunga kozi ya mafunzo kwa waamuzi yaliyofanyika jana Fit Poa Gym iliyopo Masaki, Dar es Salaam.

Saleh amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza taaluma ya waamuzi kufahamu sheria na kanuni za mchezo huo na namna ya kutoa majibu sahihi.

"Tumefunga mafunzo hayo ambayo yalifanyika kwa siku tatu kwa dhumuni la kuongeza taalum kwa waamuzi wetu ambao kila siku kumekuwa na kilio katika sekta hii," amesema Saleh.

Kaimu Mwenyekiti huyo amesema, kumekuwa na malalamiko kwa waamuzi juu ya kutoa majibu ambayo si ya kweli, hivyo wameona ni muhimu kuwapatia mafunzo.

"Nina imani mafunzo hayo yatasaidia waamuzi wetu kufanya kazi yao vizuri na kutoa majibu ambayo hayakuwa na mkanganyiko kwa mabondia wetu. Suala la waamuzi sio Tanzania peke yake ni Afrika nzima kuna shida hii ya utoaji wa majibu kwa wasimamizi wa ulingoni," amesema Saleh.

Mkufunzi wa mafunzo hayo, John Chagu ambaye ni mwamuzi wa kimataifa amesema ana imani kozi hiyo italeta matunda kwa waamuzi kufanya weledi kazi zao.

"Nitakuwa nawafuatilia na kuangalia wapi wamepiga hatua, pia kozi itakuwa endelevu lengo ni kuona Tanzania tumepiga hatua katika sekta hii ya waamuzi," amesema Chagu na kuongeza kuwa, kozi hiyo itakuwa na mafanikio makubwa kwa sababu amewafundisha mambo mengi yenye weledi kubwa.

Kwa upande mwamuzi, Pendo Njau amesema kozi hiyo imemuongezea kuwa bora zaidi ana imani atasimamia vizuri mapambano atayopangiwa.

Njau amesema hivi sasa ameongezewa nondo ambayo wadau wa ngumi wataona mabadiliko makubwa kipindi akisimamia pambano.

Mwamuzi kutoka Mkoa wa Morogoro, Mohamed Mganza alitoa wito kwa waamuzi wa mikoani kutumia fursa ya kushiriki katika koiz hiyo inapotokea.