Marcio Maximo ajaribu mfumo mpya Yanga

Mfumo huo tofauti yake kubwa ni ingizo la kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho aliyekosa mechi mbili zilizopita kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu ambapo sasa atakuwa akicheza sambamba na wenzake wawili Mrisho Ngasa na Haruna Niyonzima nyuma kidogo ya mshambuliaji Genilson Santos ‘Jaja.
Muktasari:
Mfumo ambao Mwanaspoti limeushuhudia Maximo akiwapa mazoezini jana Jumatano kwenye Uwanja wa Loyola ni 4-2-3-1.
KOCHA wa Yanga, Marcio Maximo ‘The Chosen One’ ameanza kutumia mfumo mpya wa uchezaji ambao unaweza kuanza kutumika Jumapili wiki hii dhidi ya Prisons ya Mbeya.
Awali Yanga ilikuwa ikitumia mfumo wa 4-4-2 katika mechi zake na endapo utabadilishwa huleta mingine miwili ya 4-3-3 na 4-3-1-2 ambayo mara ya mwisho ndiyo iliyowaangamiza Azam FC kwa mabao 3-0 kabla ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro wikiendi iliyopita.
Mfumo ambao Mwanaspoti limeushuhudia Maximo akiwapa mazoezini jana Jumatano kwenye Uwanja wa Loyola ni 4-2-3-1. Mfumo huo tofauti yake kubwa ni ingizo la kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho aliyekosa mechi mbili zilizopita kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu ambapo sasa atakuwa akicheza sambamba na wenzake wawili Mrisho Ngasa na Haruna Niyonzima nyuma kidogo ya mshambuliaji Genilson Santos ‘Jaja.
Nyuma ya viungo hao, viungo wengine wawili watakaokuwa nyuma yao ambao ni Hassan Dilunga na Mbuyu Twite huku katika ulinzi kukiwa na mabadiliko ya mtu mmoja ambaye ni Edward Charles anayekuja kuziba nafasi ya Oscar Joshua aliye majeruhi ambapo mabeki wengine wakiwa ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’,Juma Abdul, na Kelvin Yondani.