Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maprofesa wa Ufaransa wamtibua nyongo Adi Yusuf

Muktasari:

Kupitia kituo cha televisheni cha Ufaransa LCI, Profesa Jean-Paul Mira, mkuu wa kitengo cha huduma ya wagonjwa katika Hospitali ya Cochin iliyopo Paris na Profesa Camille Locht, mkurugenzi wa utafiti huko Inserm walipendekeza ufanisi wa chanjo hiyo unapaswa kufanyiwa majaribio Afrika

MAPROFESA nchini Ufaransa ambao walikuwa wakichambua kuhusu janga la corona wamemtibua mshambuliaji wa kimataifa waTanzania, Adi Yussuf na mastaa wengine wakubwa barani Afrika kufuatia  matamshi  yasiyofaa juu ya Afrika.
Hakuna dawa ambazo zinaweza kuzuia ugonjwa wa virusi vya corona hadi sasa, lakini wanasayansi wamegundua chanjo ya BCG - inayotumika kupunguza makali ya virusi hivyo.
Kupitia kituo cha televisheni cha Ufaransa LCI, Profesa Jean-Paul Mira, mkuu wa kitengo cha huduma ya wagonjwa katika Hospitali ya Cochin iliyopo Paris na Profesa Camille Locht, mkurugenzi wa utafiti huko Inserm walipendekeza ufanisi wa chanjo hiyo unapaswa kufanyiwa majaribio Afrika.
“Huo ni upuuzi ambao haupaswi kufumbiwa macho, Afrika sio sehemu ya kufanyia majaribio,” alisema Adi ambaye ni mchezaji wa Blackpool anayeichezea Boreham Wood kwa mkopo. Kauli hiyo pia  ilimchukiza mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Inter Milan na FC Barcelona, Samuel  Eto’o ambaye alitumia mtandao wa kijamii kuandika: “Afrika sio uwanja wako wa kucheza.”
Nyota wa kimataifa wa Senagel, Demba Ba alionekana kukerwa na msomi huyo kwa kuandika: “Karibu Magharibi ambapo watu weupe wanajiamini kuwa bora zaidi kwamba ubaguzi wa rangi na ujasusi huwa kawaida. Wakati wa kuinuka.”
Kiungo wa zamani wa Ufaransa na Inter Milan, Olivier Dacourt aliandika kwa kuuliza, ”Je! ni kweli wapo siriazi?”.