Mangalo, Mtibwa bado kidogo tu

Muktasari:
- Mangalo ambaye alikuwa anajiuguza goti alirejea kwenye uwanja wa mazoezi tangu dirisha dogo la msimu ulioisha lakini hakupata ofa ambayo ingemfanya arudi uwanjani.
BAADA ya kukaa nje ya uwanja msimu mzima akiuguza jeraha la goti, beki wa zamani wa Biashara United na Singida Foutain Gate, Abdulmajid Mangalo yupo kwenye hatua za mwisho kumalizana na Mtibwa Sugar.
Mangalo ambaye alikuwa anajiuguza goti alirejea kwenye uwanja wa mazoezi tangu dirisha dogo la msimu ulioisha lakini hakupata ofa ambayo ingemfanya arudi uwanjani.
Chanzo cha kuaminika kutoka Mtibwa Sugar ambayo imepanda daraja msimu huu kimeliambia Mwanaspoti kuwa mazungumzo baina ya pande zote mbili yanaenda vizuri na muda wowote beki huyo anaweza kusajili mkataba wa miaka miwili.
“Ofa yetu wake ni miaka miwili tunataka kurudi imara na kuwa na timu shindani msimu ujao hivyo tunachoingatia ni ubora na uzoefu ili kuwa na timu ambayo itarudisha mashabiki ambao tuliwapoteza baada ya kushuka daraja,” alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza;
“Licha ya kutokuonekana uwanjani kwa muda kutokana na kuuguza jeraha lake goti tumejiridhisha kabla ya kumsainisha mkataba kilichobaki ni makubaliano tu yakienda sawa tutamalizana.”