Man United yasubili zari kumnasa Bale

Muktasari:

Real Madrid itavaa Juventus kwenye Uwanja wa Cardiff hapo Juni 3, na nyota huyo wa zamani wa Tottenham hajacheza tangu alipoumia wakati wa mchezo dhidi ya Barcelona, lakini anategemewa kuwa fiti kabla ya fainali hiyo.

Manchester United itaanza harakati kumnasa Gareth Bale kama hatoanza katika kikosi cha Real Madrid kitakachocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus.

Real Madrid itavaa Juventus kwenye Uwanja wa Cardiff hapo Juni 3, na nyota huyo wa zamani wa Tottenham hajacheza tangu alipoumia wakati wa mchezo dhidi ya Barcelona, lakini anategemewa kuwa fiti kabla ya fainali hiyo.

Hata hivyo, Isco amekuwa moja wa wachezaji nyota na amefanikiwa kuliziba vizuri pengo la Bale.

Endapo Bale ataachwa nje na Zinedine Zidane katika kikosi cha kwanza kitakachocheza nyumbani kwao, gazeti la Mundo Deportivo limedai kuwa Man United wanaamini watakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kumsaji nyota huyo.

Florentino Perez alivunja benki kwa kumnunua Bale kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia 2013.

Hata hivyo, uwepo wa Cristiano Ronaldo umeonekana kuwa kizingiti kwa Bale kutamba pamoja na kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.