Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makata atupwa nje, Mtupa kuiongoza Prisons dhidi ya Yanga

Muktasari:

  • Makata alitua Prisons akitokea Pamba Jiji ya Mwanza, ambapo ameongoza michezo 14 akishinda miwili, sare tano na kupoteza saba.

Licha ya uongozi kutothibitisha moja kwa moja, lakini habari za uhakika ni kuwa Tanzania Prisons imemtema aliyekuwa kocha mku wa kikosi hicho, Mbwana Makata na msaidizi wake, Renatus Shija.

Badala yake Shaban Mtupa ndiye ataanza kusimamia kikosi hicho na leo Jumatano, Desemba 18 amesimamia mazoezi ya wachezaji kujiandaa na mechi ijayo dhidi ya Yanga.

Makata na msaidizi wake walitua kikosini humo mwanzoni mwa msimu huu, ambapo timu haikuwa na matokeo mazuri wakiwa nafasi ya 15 kwa pointi 11 baada ya michezo 14.

Imeelezwa kuwa katika kikao cha usiku wa kuamkia leo, uongozi wa Maafande hao, ulikubaliana na Makata kuachana kwa maslahi mapana ya timu kutokana na mwenendo wa matokeo kutoridhisha.

Mwanaspoti iliwatafuta baadhi ya viongozi wa timu hiyo, lakini hakuna aliyepokea simu kufafanua uamuzi huo na hatma ya Prisons katika michezo ijayo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mtupa amekiri kukabidhiwa majukumu, akieleza kuwa katika mazoezi ya leo asubuhi, ameona utayari wa wachezaji katika mechi zinazofuata.

Amekiri ugumu kuwepo akieleza kuwa hawezi kuzikimbia changamoto, akibainisha kuwa bado muda upo kubadili upepo haswa wakati huu wa dirisha dogo.

"Najua mechi ijayo ni dhidi ya Yanga ugenini, nimeona vijana wana ari na morali, tutaenda kupambana na kufanyia kazi sehemu yenye upungufu haswa dirisha dogo ili kufanya vizuri.

"Tumeandamwa sana na majeruhi kikosini, lakini tutaboresha, nina uzoefu na timu na lolote linawezekana, tupeane sapoti na muda," amesema Mtupa.

Prisons inatarajia kuwa uwanjani kukipiga dhidi ya Yanga, Desemba 22 mwaka huu, mchezo utakaopigwa Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam, ukiwa wa kumaliza mzunguko wa kwanza kwa 'Wajelajela' hao.