Makamu wa Rais SMZ aongoza mazishi ya baba yake Ghalib

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Themed Suleiman Abdullah ameshiriki mazishi ya Baba mzazi wa mfadhili wa Yanga Ghalib Said Mohamed, marehemu Said Mohamed sambamba na mamia ya waombolezaji mbalimbali.
Abdula amefika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam akiwa sambamba na Ghalib ambapo pia Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu.
Wadau mbali wa Soka kutoka taasisi mbalimbali wakiwemo Rais wa TFF Wallace Karia na kikosi kizima cha Yanga nao walikuwa katika umati huo katika mazishi hayo yaliyofanyika leo jioni.
Marehemu Said Mohamed alifariki alfajiri ya kuamkia leo huku Ghalib akiwa safarini ambapo alirejea jana mchana na kuwahi mazishi hayo.
Kocha wa Yanga Nesreddine Nabi amesema walilazimika kubadili ratiba yao ya mazoezi jana kuhakikisha wanakwenda kushiriki mazishi ya baba wa Mfadhili wao.
"Timu nzima iliona kuna haja ya kuharibu ratiba kwa ajili ya kushiriki ibada ya mazishi,sisi tunajua jinsi Ghalib alivyokuwa karibu na hii timu wakati wote tulistahili kuwa hapa," amesema Nabi.