Makambo kutua Dar

Dili la mshambuliaji, Heritier Makambo limeiva na wakati wowote kabla ya Jumatatu atakuwa nchini kuja kusaini rasmi Yanga ambako amesema ni nyumbani.

Makambo kuanzia jana alikuwa anasubiri tiketi ya ndege tu aje nchini kurudisha mabao yake.

Straika huyo aliachana na Horoya ya Guinea kiroho safi wikichache zilizopita na kuliambia Mwanaspoti kwamba anakuja Jangwani kwani ameshazungumza kwa kirefu na viongozi. Yanga mpaka sasa imeshamalizana na Dickson Ambundo na David Brayson ambayo tayari wapo kwenye kikosi cha Kagame .