Magori aibukia ubunge Afrika Mashariki

Friday August 05 2022
Magori PIC
By Ramadhan Hassan
By Lewis Mujemula

Dodoma. Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa klabu ya Simba, Crescentius Magori ni mmoja ya waliojitokeza kuomba ridhaa ya CCM kuchaguliwa kugombea ubunge wa Afrika Mashariki.

Magori ambaye pia ni mshauri wa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Simba amechukua fomu hiyo leo ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti  5, 2022 Jijini Dodoma Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Oganaizesheni, Maudline Castico amesema mbali na Magori wanachama wengine 94 wameomba  ridhaa ya kugombea  nafasi hizoo ndani ya chama.

Ongezeko la wanachama hao limezidi kuongeza joto la uchaguzi huo kwani nafasi zinazohitajika ni tisa tu lakini wagombea wamefika 94 na kuna uwezekano wakaongezeka kwani siku ya mwisho kuchukua fomu ni Agosti 10.

Advertisement