Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mafunzo yashushwa kileleni, vita ya ubingwa ZPL yachukua sura mpya

Muktasari:

  • Timu ya Mafunzo imeshushwa kutoka kileleni hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) baada ya kufungwa bao 1-0 na Mlandege ambayo kwa sasa inaongoza ligi ikifikisha alama 56, jambo ambalo limefanya vita ya kuwania ubingwa msimu huu wa 2024-25 kuchukua sura mpya zikisalia mechi mbili.

KIPIGO cha bao 1-0 ilichopokea Mafunzo FC kutoka kwa Muembe Makumbi City katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliofanyika jana Mei 30, 2025 kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja, kimeifanya timu hiyo kushushwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Wakati Mafunzo ikishushwa kutoka kileleni hadi nafasi ya tatu ikiwa na alama 54, Mlandege kwa sasa inaongoza ligi baada ya kuifunga KMKM mabao 3-1, mchezo uliofanyika pia jana kwenye Uwanja wa Mao B, Unguja.

Ushindi wa Muembe Makumbi ulioifanya timu hiyo kutoka nafasi ya nne hadi ya pili ikifikisha alama 55, ulitokana na bao la dakika ya 87 lililofungwa na Khelef Naim.

Licha ya Muembe Makumbi kushinda mchezo huo, lakini Mafunzo ilionekana kuutawala tangu dakika ya kwanza lakini itajialaumu kwa kupoteza nafasi nyingi ambazo kama ingezitumia vizuri ingeondoka na ushindi.

Kwa upande wa Mlandege iliyopo kileleni na alama 56, mshambuliaji wa timu hiyo, Abdallah Iddi 'Pina' ameendelea kujiwekea heshima katika msimamo wa ufungaji akifanikiwa kufikisha mabao 18 wakati wakiifunga KMKM.

Pina alifunga bao la mwisho dakika ya 90+2, kabla ya hapo, Bashir Suleiman alianza kuzitikisa nyavu za KMKM dakika ya 37, kabla ya Mukrim Hassan kuisawazishia KMKM dakika ya 43 na kwenda mapumziko timu hizo kuwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili wakati zikisalia dakika 15 mchezo kumalizika, Suleiman Kidawa aliifungia bao Mlandege dakika ya 75, kisha Pina akahitimisha ushindi huo.

Ligi hiyo inayoelekea ukingoni huku timu nyingi zikicheza mechi 28 na kubakiza mbili, leo Mei 31, 2025 inaweza kuwa nafasi nzuri kwa KVZ kutoka nafasi ya nne hadi ya pili endapo itaibuka na ushindi dhidi ya Uhamiaji kwenye Uwanja wa Mao A. Kwa sasa KVZ inashika nafasi ya nne ikiwa na alama 53 baada ya kucheza mechi 27.

Timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo zinachuana vikali katika kuwania ubingwa msimu huu na mechi zilizobaki zimebeba maana kubwa kwa kila moja.

Mafunzo mechi mbili zilizobaki ni dhidi ya Junguni United na Chipukizi ambazo zipo katika mapambano ya kuepuka kushuka daraja msimu huu.

Mlandege nayo imebakiza mechi dhidi ya Kipanga na New City, huku Muembe Makumbi ikicheza dhidi ya KVZ na Malindi.

Kwa upande wa KVZ ambayo leo inacheza dhidi ya Uhamiaji, baada ya hapo itakabiliana na Muembe Makumbi na Kipanga.