Prime
Machezo: Maxi hakabiki kirahisi

Muktasari:
- Timu hizo zilikutana mapema wiki hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, huku Maxi akiendelea kutoa shoo ya maana akifunga mabao mawili na Machezo anasema licha ya kukabana na viungo wawili mahiri, Mudathir na Aziz KI, lakini aliyewatesa zxaidi ni Maxi.
KIUNGO wa JKT Tanzania, Hassan Nassor Maulid ‘Machezo’ aliyesimama kati na kuchuana na Mudathir Yahya na Stephane Aziz Ki wa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara na timu hiyo kupigwa mabao 5-0, alisema hakuna mchezaji aliyewanyima raha kama Maxi Nzengeli aliyedai hakabiki uwanjani.
Timu hizo zilikutana mapema wiki hii kwenye Uwanja wa Azam Complex, huku Maxi akiendelea kutoa shoo ya maana akifunga mabao mawili na Machezo anasema licha ya kukabana na viungo wawili mahiri, Mudathir na Aziz KI, lakini aliyewatesa zxaidi ni Maxi.
“Mimi nilikuwa sina bato yoyote na Aziz Ki au Mudathir, nilichokuwa nafanya ni kutekeleza majukumu niliopewa na kocha, ila aliyetusumbua ni Maxi, kwani jamaa hakabiki kabisa,” alisema Machezo.
Alisema mara nyingi alikuwa akijaribu kumkaba Maxi lakini hata ukimfanyia press unakuta keshatoa mpira mguuni kwake tofauti na wachezaji wengine
“Nikiri wazi kwamba aliyenipa tabu kwenye mchezo huo ni Maxi kwa sababu hata ukimfanyia press unakuta keshatoa mpira, ila kwa Aziz Ki nilimsoma vizuri alikuwa na chenga moja tu na Muda namuona wa kawaida, ndio maana namtaja aliyetusumbua, Maxi anajua sana,” alisema kiungo wa zamani wa Mbeya City.