Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabosi wapya BD Februari 22

BD Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa Emesu, katika uchaguzi huo Mwenyekiti na Katibu watakaochaguliwa watapata nafasi ya kwenda kuchagua viongozi wa Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF) Februari 28 mwaka huu, mkoani Dodoma. Kwa sasa Mwenyekikiti wa DB ni Shendu Mwangala na katibu akiwa ni Mpoki Mwakipake.

MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), Okare Emesu, amesema chama hicho kinatarajia kupata viongozi wapya kupitia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Februari 22 mwaka huu.

Hata hivyo, Emesu amesema eneo litakalotumika kwa uchaguzi huo litatangazwa baadaye, ila maandalizi yameshaanza kwa ajili ya tukio hilo.

Emesu aliliambia Mwanaspoti, uchaguzi huo ulishindwa kufanyika mapema mwaka huu kutokana na Ligi ya Kikapu ya Daraja la Kwanza Mkoa wa Dar es Salaam iliyokuwa inaendelea.

Baada ya hapo, Kamati ya Michezo ya Mkoa Dar es Salam yenye jukumu la kuratibu kamati ya kusimamia uchaguzi huo, iliteua wajumbe wa kamati ya uchaguzi wa DB ambao ni yeye (Okare Emesu) ambaye ni Mwenyekiti akisaidiwa na; Seif Ngowi (Katibu) na wajumbe Bahati Mgunda, Amin Mtambo na Gerald Gulaka.

Kwa mujibu wa Emesu, katika uchaguzi huo Mwenyekiti na Katibu watakaochaguliwa watapata nafasi ya kwenda kuchagua viongozi wa Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF) Februari 28 mwaka huu, mkoani Dodoma. Kwa sasa Mwenyekikiti wa DB ni Shendu Mwangala na katibu akiwa ni Mpoki Mwakipake.

“Kwa kweli bila ya kufanya uchaguzi, mkoa wa Dar es Salaam ungeweza kukosa uwakilishi wa kuingia kuchagua viongozi wa TBF,” amesema.

Emesu alitaja nafasi zitakazowaniwa katika kinyang’anyiro hicho kuwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Kamishina wa Mipango ya Maendeleo, Kamishina wa Watoto na Maendeleo ya Vijana.

Nafasi nyingine ni; Kamishina wa Watu wenye Ulemavu, Kamishina wa Tiba ya Wanamichezo na Kamishina wa Ufundi na Mashindano.