Mabaunsa wazua utata kwa Manara

Saturday September 25 2021
mabaunsa pic
By Thomas Ng'itu

MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amejikuta katika wakati mgumu yeye na viongozi wenzake baada ya kuzuiwa kuingia uwanjani pale mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga kumalizika.

Mpira ulipomalizika viongozi wa Yanga walishuka chini kwa lengo la kwenda kuwapongeza wachezaji wao kisha walitaka kwenda uwanjani kwa lengo la kushuhudia ugawaji wa zawadi.

Wakati wakiwa wanataka kupita katika lango la kuingilia uwanjani mabaunsa wakaanza kuwazuia.

Mwanaspoti lilishuhudia Manara akiwa na mabaunsa wake wakivutana na wale wa uwanjani.

Wakati huo huo Injinia Hersi Said yeye alikuwa yupo kwa pembeni na viongozi wemgine na walipoona hali sio shwari waliamua kuondoka huku wakishangilia na kwenda kupita mlango ambao huwa wanapaki magari ya wagonjwa (Ambulance).

Manara alianza kuwa katika wakati mgumu tangu alipokuwa VVIP Mwanaspoti lilishuhudia akitolewa baada ya kuwa anashangilia mara kwa mara.

Advertisement

Manara alisikika anasema;"Haya semeni tena sasa, nasema semeni tena sasa."

Advertisement