Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabao ya vichwa yaitesa Simba SC

Muktasari:

Simba itakuwa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu kesho dhidi ya Azam FC, kabla ya kuifuata AS Vita. Simba itakuwa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu kesho dhidi ya Azam FC, kabla ya kuifuata AS Vita.

Dar es Salaam. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, Simba inashuka uwanjani kesho kuivaa Azam FC katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo ni wa kiporo, sawa na ule wa juzi walioibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji, uliofanyika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Baada ya mchezo huo wa kesho, Simba itakuwa ikijiandaa na safari ywa kwenda DR Congo kuivaa miamba ya soka ya nchini hiyo, AS Vita, katika mchezo wa kwanza wa Kundi A wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inashuka dhidi ya AS Vita, ikiwa na kumbukumbu mbaya ya mchezo wa ugenini dhidi ya kikosi hicho cha kocha Florent Ibenge, kwani misimu miwili iliyopita ilichakazwa mabao 5-0.

Katika mchezo huo na mingine kadhaa, Simba ilionyesha udhaifu wa kushindwa kucheza mipira ya kona, kitu ambacho kimeendelea kuigharimu miamba hiyo katioka meche kadhaa.

Simba imerufuhusu mabao sita hadi sasa katika Ligi Kuu Tanzania Bara, wakati matatu ikifuingwa kwa kichwa dhidi ya Tanzania Prisons, Mtibwa Sugar na lile la juzi dhidi ya Dodoma Jiji.

Katika mashindano ya Simba Super Cup, miamba hiyo iliruhusu bao moja pekee, ambalo nalo lilifungwa kwa kichwa walipoilaza Al Hilal mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Simba bado ina shida katika kucheza mipira ya kona na krosi ama mikwaju ya adhabu inayopigwa kutoka pembeni, jambo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi haraka kabla ya kukutana na AS Vita.

Kwenye kulipatia tiba hilo, Simba wamemsajili beki wa kati, Peter Muduhwa ili aje kutumika katika mashindano ya kimataifa, lakini ni majeruhi.

Simba pia wanamkosa, John Bocco na Chriss Mugalu kutokana na majeraha, kwa maana hiyo amebaki, Meddie Kagere mwenyewe katika eneo la ushambuliaji, ambaye akikutana na mabeki wenye uwezo wa kukaba kama wale wa TP Mazembe hushindwa kuonyesha makali yake.

Katika hilo, Simba ilimsajili, Junior Lokosa, ambaye tangu kufika kwake katika kikosi hicho ameonekana kutokuwa fiti na hata kushindwa kutoa ushindani kwa timu pinzani.

Kwa jinsi ambavyo Lokosa ameonekana katika mazoezi na mechi dhidi ya TP Mazembe aliyocheza, bado anahitaji muda wa kujiandaa zaidi na mkataba wake wa miezi sita aliosaini hapo anaweza kujikuta umemalizika huku akiwa bado hajawa msaada.

Shida nyingine ya Simba ni baadhi ya wachezaji kama Bernard Morrison, Clatous Chama na wengineo ambao wanacheza zaidi kwa kuwafurahisha mashabiki kuliko mahitaji ya timu, wachezaji watano wanaocheza katika safu ya ushambuliaji si wakabaji pia.

Simba inaposhambulia, zoezi la kukaba mara nyingi linaanzia kwa Taddeo Lwanga na wachezaji waliokuwa nyuma yake kwa maana hiyo wakikutana na timu yenye wachazaji bora kwenye kushambulia lazima watakutana na mtihani mgumu kuwazuia.

Ubora ambao Simba wameonyesha chini ya kocha, Didier Gomes inacheza zaidi kwa kumiliki mpira muda mwingi, kushambulia zaidi na hili linaweza kuwa faida kwao wakiwa nyumbani na uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja.

Gomes alisema kikosi chake kimeonyesha makosa ambayo wanatakiwa kuyafanyia kazi ili kuwa bora katika michezo inayofuata.

“Ndiyo maana nipo hapa tutakwenda kuyafanyia kazi makosa yetu katika mazoezi ili kubadilika na kuwa bora zaidi, lakini kiujumla nimeridhika na viwango,” alisema Gomes.

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Edo Kumwembe alisema Simba wana kikosi kizuri wakichagizwa na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, jambo ambalo kwa timu za ndani si rahisi kupoteza dhidi yao.

“Upungufu na shida ambazo Simba kwa mashindano ya ndani ni ngumu kuonekana mara kwa mara ila wanatakiwa kuyarekebisha na kuyafanyia kazi kwani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hakuna mzaha,” alisema Edo.