Mabango ya ubingwa wa Liverpool yatupwa ‘jalalani’

Muktasari:

  • Mwishowe mapambo na majukwaa ya Liverpool yaliwekwa kando kupisha wababe wa England msimu wa 2018/19 Man City kutawazwa mabingwa.

Unaweza kusema labda tusubiri msimu ujao. Hii imetokea jana wakati timu za Manchester City na Liverpool wakiwa kwenye mbio za ubingwa, ambapo Chama cha Soka England kilikuwa kimeshaweka mazingira kwa timu yoyote ambayo ingeibuka na ushindi kwa ajili ya kupamba jukwaa uwanjani.

Upande wa Machester City kwenye uwanja wa Amex, kulikuwa na majukwaa na mapambo yenye jina la timu hiyo huku kwenye dimba la Anfield yalikuwa yamewekwa tayari iwapo timu hiyo ingetwaa taji la ubingwa.

Licha ya Liverpool kuifunga timu mabao Wolverhampton mabao 2-0 lakini ubingwa ulikwenda kwa Manchester City  ambao wamemalizia kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na tofauti ya alama ya pointi moja.

Mwishowe mapambo na majukwaa ya Liverpool yaliwekwa kando kupisha wababe wa England msimu wa 2018/19 Man City kutawazwa mabingwa.

Matokeo kwa mechi zingine yalimalizika kama ifuatavyo; Fulham 0-4 Newcastle United, Bunley 1-3 Arsenal, Crystal Palace 5-3 AFC Bournemouth, Leicester City 0-0 Chelsea. Pia Machester United 0-2 Cardiff City, Tottenham 2-2 Everton, Watford 1-4 West Ham, Southampton 1-1 Huddesfield