Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabadiliko Simba yala vichwa 15

Muktasari:

Simba mpaka sasa imethibitisha kusajili wachezaji tisa huku pia ikifanya mazungumzo na straika Mzambia, Walter Bwaya na kiungo raia wa Uganda, Antony Mawejje.

SIMBA ipo katika harakati za kuboresha kikosi chake kuelekea kwenye mashindano ya kimataifa mwakani, lakini wimbi hilo limepita na vichwa 15 ambavyo vimepunguzwa ili kupisha nguvu mpya.

Mabadiliko ambayo wameyafanya washindi hao wa Kombe la Shirikisho (FA), yamewaondoa wachezaji 13 huku watendaji wawili wa benchi la ufundi nao wakitolewa. Meneja Mussa Hassan ‘Mgosi’ amepelekwa kuwa kocha wa timu ya vijana na kocha wa makipa, Iddi Salim mkataba wake ukiwa umemalizika.

Simba mpaka sasa imethibitisha kusajili wachezaji tisa huku pia ikifanya mazungumzo na straika Mzambia, Walter Bwaya na kiungo raia wa Uganda, Antony Mawejje. Lakini Bwalya dili lake linaonekana kuwa gumu kwa vile anataka dau kubwa na gharama za kuvunja mkataba wake pia ni nzito ingawa Simba bado haijakata tamaa.

Katika orodha ya wachezaji 13 ambao hawatavaa jezi nyekundu na nyeupe msimu ujao, wapo wanne ambao wametimkia timu nyingine. Nyota hao ni Ibrahim Ajibu aliyetua Yanga, Abdi Banda aliyejiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini, Pastory Athanas aliyepelekwa Singida United na Peter Manyika ambaye klabu imepanga kumpeleka Lipuli kwa mkopo.

Mabadiliko hayo yanawahusu kipa Daniel Agyei ambaye mabosi wa Simba hawakuridhishwa na kiwango chake msimu uliopita na wamepanga kumtoa ambapo nafasi yake imezibwa na kipa bora wa Ligi Kuu, Aishi Manula.

Mabeki Janvier Bokungu, Novatus Lufunga, Malika Ndeule na Hamad Juma wanaachwa kutokana na viwango vyao kutofikia malengo ya klabu ambapo nafasi zao zitazibwa na Shomary Kapombe, Ally Shomary, Yusuf Mlipili na Salim Mbonde ambao tayari wamesaini.

Kwa upande wa viungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto amepitiwa pia na panga. Winga Jamal Mnyate anaachwa baada ya kucheza kwa kiwango duni msimu uliopita huku chipukizi, Hija Ugando akiwa ameomba kuachwa baada ya kuona hana nafasi ya kuwatumikia mabingwa hao mara 18 wa Ligi Kuu.

Omog ambakiza Mayanja

Juzi Jumapili viongozi wa Simba walikubaliana kwamba Kocha Msaidizi, Jackson Mayanja asepe na nafasi yake apewe Etienne Ndayiragije wa Mbao FC. Lakini walipompelekea taarifa rasmi kocha mkuu Joseph Omog, akagoma na akasisitiza kuwa hayuko tayari kufanya kazi na kocha msaidizi mpya.

Mabosi wa Simba kwa pamoja walikubaliana kwamba Mayanja hafai kuendelea kumsaidia Omog kwani walihitaji kocha wa kiwango cha juu zaidi ambapo walimpendekeza Ndayiragije ambaye walishaanza naye mazungumzo, lakini sasa wameufuta mchakato huo na jana Jumatatu Manyanja aliingia kazini kama kawaida.

Habari zisizo na mashaka ambazo Mwanaspoti imezinasa ni kwamba, Omog amewaambia mabosi hao kama wanamwondoa Mayanja basi wajiandae kumfuta kazi na yeye jambo ambalo wameona ni kamari na halitawasaida, hivyo kusitisha mpango wa Ndayiragije. Kocha huyo amewambia viongozi kwamba mafanikio aliyoyapata Simba yalitokana na misingi ya Mayanja ambayo kwa mtu ambaye hana uelewa wa kiufundi hawezi kubaini, ndio maana viongozi wakanywea.