Lyanga, Mahadhi kuongoza jeshi la Geita

KOCHA Etiene Ndayiragije wa Geita Gold amewaanzisha washambuliaji Juma Mahadhi na Daniel Lyanga katika eneo la ushambuliaji kwenye mchezo dhidi ya Yanga utakaochezwa saa 1:00 usiku leo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Lyanga ni miongoni mwa washambuliaji hatari na msimu uliopita akiwa na JKT Tanzania aliifungia timu hiyo mabao tisa, huku upande wa Mahadhi yeye alipokuwa na Ihefu ni kama alikuwa anarejea kwenye ubora wake baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kisa majeraha.
Kwenye kikosi hicho pia kiungo Maka Edward ambaye alishacheza Yanga na soka la kulipwa nchini Morocco katika klabu ya Moghreb Toutan na msimu huu amerejea tena nchini.
Pia katika upande wa beki yupo Oscar Masai ambaye msimu uliopita aliichezea timu ya Ihefu Fc ambayo imeshuka daraja.
Kikosi kilichoanza ni Khomeinh Abubakar, Derick Mussa, Amosi Kidikilo, Chilo Mkama, Oscar Masai, Yusph Kagoma, Kalagha Mbindo.
Wengine ni Raymond Massota, Daniel Lyanga, Maka Edward na Juma Mahadhi.