Luis Suarez aanza kwa kuweka rekodi Atletico

Tuesday September 29 2020
chelsea pic

Mdirid, Hispania. Chelsea ipo tayari kumtoa kwa mkopo kipa wake, Kepa, baada ya kumsajili nyota wa Rennes, Edouard Mendy na kuandaliwa kuwa chaguo la kwanza.

Luis Suarez amefunga mabao mawili akitokea benchi katika mchezo wake wa kwanza kuitumikia klabu yake mpya ya Atletico Madrid juzi usiku dhidi ya Granada.

Pasi ya mwisho ya bao alimlisha Marcos Llorente, ambaye aliifungia Atletico bao la nne, licha ya kutokea benchi kipindi cha pili.

Ilimchukua Suarez dakika 15 kufunga bao lake la kwanza akiwa katika jezi nyingine mpya, akimalizia kwa kichwa mpira wa krosi dakika ya 85.

Mambo yalizidi kuwa mazuri kwa nyota huyo wa zamani wa Liverpool, wakati alipofunga bao lake jingine dakika nane kabla ya mchezo kumalizika akihitimisha ushindi wa mabao 6-1 kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano.

Advertisement