Lomalisa apewa Polisi

KOCHA wa Yanga, Nesreddine Nabi amemuanzisha kwenye kikosi cha kwanza, beki mpya Joyce Lomalisa aliyesajiliwa kutoka Sagrada Esperanca ya Angola.
Yanga inacheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania ambayo msimu uliyoisha waliichapa nyumbani na ugenini.
Mashabiki wa Yanga leo Agosti 16, 2022, wataona live kiwango cha beki wao kushoto Lomalisa ambaye hakupangwa na kocha kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, timu hiyo ikishinda mabaon 2-1 dhidi ya Simba.
Nafasi aliyopangwa Lomalisa anacheza Kibwana Shomari na Farid Mussa ambaye ameanzia benchi.
Akifanikiwa kuonyesha kiwango cha juu, atakuwa ametangaza ushindani wa namba mbele ya wenyeji wake Shomari na Faridi ambao kwa muda waliyoitumikia Yanga wamecheza kwa kiwango kikubwa.
Kikosi cha Yanga kinachoanza dhidi ya Polisi Tanzania wenyeji wa mchezo huo ni Djigui Diarra, Shaban Djuma, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Khalid Aucho, Gael Bigirimana, Jesus Moloko, Fiston Mayele,Stephane Aziz Ki na Dickson Ambundo.
Kikosi cha akiba ni Abdultwalib Mshery,Yanick Bangala, Ibrahim Bacca,Zawadi Mauya, Abubakar Salum 'Sure Boy', Fisal Salum 'Fei Toto', Bernard Morrison, Farid Mussa na Heritier Makambo.