Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Kuu Wanawake kuendelea kibabe leo

Muktasari:

  • MZUNGUKO wa sita wa Ligi Kuu ya Soka ya  Wanawake (WPL) unatarajiwa kuendelea leo Jumatano huku mchezo unaosubiriwa kwa hamu ukiwa ni Derby ya Dodoma kati ya Fountain Gate Princess dhidi ya Baobab Queens.

MZUNGUKO wa sita wa Ligi Kuu ya Soka ya  Wanawake (WPL) unatarajiwa kuendelea leo Jumatano huku mchezo unaosubiriwa kwa hamu ukiwa ni Derby ya Dodoma kati ya Fountain Gate Princess dhidi ya Baobab Queens.

Mchezo huo namba 27 unaotarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Mpaka sasa JKT Queens inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 13 ikifuatiwa na Fountain Gate Princess yenye pointi 12 na Mkwawa Queens inaburuza mkia ikiwa na pointi moja.

Msimu uliopita Boabab Queens ilipoteza michezo yote miwili kwa Fountain ikikubali kichapo cha mabao 3-1 katika mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili wakifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Fountain Gate Arena.

Oktoba 22 mwaka jana, katika  Tamasha la Wanawake lilofanyika  katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, Baobab Queens waliibuka na ushindi kwa penalti 8-7 baada ya ndani ya dakika 90 timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1.

Baobab inamtegemea mshambuliaji wake Jamila Rajabu ambaye katika michezo mitano amefunga mabao mawili huku Fountain ikimtegemea Mkenya Cynthia Musungu ambaye amefunga mabao manne katika michezo mitano.

Kocha wa Fountain Gate Princess, Alex Alumirah alisema kikosi chake kipo vizuri na hakuna majeruhi na wamejipanga kupata ushindi huku Kocha wa Baobab Queens Juma Ikaba akisema   atawakosa, Rahma Salim na Semeni Salanga ambao ni majeruhi.

Mchezo mwingine unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Chuo cha Mkwawa mkoani Iringa kwa Ceasiaa Queens kuwakaribisha Yanga Princess.

Ceasiaa Queens wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wakiwa na pointi sita huku Yanga Princess wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 10.

Katika mchezo huo kwa mara ya kwanza anaweza kuanza mshambuliaji mpya wa Yanga Princess Cidalia Cuta, ambaye amesajiliwa kutokea nchini Msumbiji.

Ceasiaa Queens tayari imepata vibali vya wachezaji wa kigeni Tessy Biahwo,(Nigeria) Grace Mbelai, Tastine Mushiwa (Congo, Akujo Ester, Mariamu Musubika, Immaculate Kizza, Miriamu Ibonyo (Uganda).

Kocha wa Ceasiaa Queens, Mustapha Kayinda alisema hakuna majeruhi kwenye kikosi chake ila utakuwa mchezo mgumu lakini wamejipanga kupata matokeo huku akiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Kocha wa Yanga Princess, Sebastin Nkoma alisema mshambuliaji wake Aniella Uwimana, anaendelea vizuri na anaweza kumtumia katika mchezo huo.

Michezo mingine inayotarajiwa kupigwa leo Alliance Girl watakawakaribisha Mkwawa Queens ya mkoani Iringa, katika uwanja wa Nyamagana na Amani Queens ya mkoani Lindi watawakaribisha mabingwa watetezi Simba Queens katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Kipute kingine vinara wa ligi hiyo, JKT Queens watawakaribisha The Tiger ya Jijini Arusha katika mchezo unaotarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Meja Generali  Isamuhyo.