Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi Bara vita yahamia hapa

Muktasari:

  • Vita ya kusaka mshindi wa tatu inazihusisha Singida Big Stars yenye pointi 51, ikipishana pointi moja na Azam FC iliyo nafasi ya nne na kila timu ikisaliwa na mechi nne na timu yoyote itakayozichanga vyema karata zake inaweza kunyakua nafasi hiyo na kuvuta mkwanja wa maana wa Azam Media.

LIGI Kuu Bara imebakiza michezo minne kumalizika huku watetezi Yanga ikiongoza msimamo kwa kukusanya pointi 68 na michezo mitano, ilihali Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 60, lakini kuna vita mpya imehamia kwenye kusaka nafasi ya tatu na eneo la mkiani kwenye eneo la kushuka daraja.

Vita ya kusaka mshindi wa tatu inazihusisha Singida Big Stars yenye pointi 51, ikipishana pointi moja na Azam FC iliyo nafasi ya nne na kila timu ikisaliwa na mechi nne na timu yoyote itakayozichanga vyema karata zake inaweza kunyakua nafasi hiyo na kuvuta mkwanja wa maana wa Azam Media.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu uliopita (2021/22), hatua ya 26 Yanga ilikuwa ikiongoza kwa pointi 64 tofauti ya pointi 13 na Simba, huku Namungo ilikuwa y tatu na pointi 37 sawa na Azam iliyomaliza ya nne.

Katika misimu minne mfululizo mwaka 2019-2023, Simba na Yanga zimekuwa zikimaliza kwenye nafasi mbili za juu zikipishana kutwaa ubingwa, huku nafasi ya tatu na nne zikiziachia msala timu nyingine na Azam ikiwa moja ya timu hizo.

Hadi hatua ya 26 msimu uliopita, Yanga haikuwa imepoteza mchezo wowote kabla ya rekodi hiyo kuharibiwa na Ihefu Fc msimu huu baada ya kuichapa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Highland Estate.

Simba yenyewe ilipoteza michezo miwili msimu iliopita hadi kufikia hatua hiyo na msimu huu imepoteza mmoja hadi sasa kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam.

Katika nafasi ya tatu msimu uliopita hatua kama hiyo ilishikiliwa na Namungo iliyo ya sita kwa sasa na kwa sasa nafasi hiyo ya tatu ikishikiliwa na Singida huku zikitofautiana kwa pointi 16, hivyo ni wazi ushindani ni mkubwa kwenye nafasi hiyo.

Nafasi ya nne misimu miwili mfululizo hatua hiyo imekamatwa na Azam na kwenye msimamo hadi sasa ina pointi 50 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, ikiwa ni tofauti ya 13 na msimu uliopita ilikuwa na  37.

Yanga ikishinda mechi zake sita zilizosalia itamaliza na alama 83 na kutetea ubingwa wake, huku watani zao itamaliza na 75 na Wanajangwani hao imepishana kwa pointi 15 na aliye nafasi ya nne (Azam) kabla ya mechi ya jana, tofauti na msimu uliopita zilitofautiana pointi 27, ikimaliza kileleni na Azam ya nne.

Lakini utamu upo kwenye eneo la kushuka daraja, kwani hakuna kitu kinachoweza kuinusuru Polisi Tanzania iliyopo mkiani na alama 19 kuweza kupona kushuka daraja au kuangukia kwenye play-off kwa michezo iliyosaliwa kabla ya kufunga msimu.

Ruvu Shooting inayaofuata juu ya Polisi nao ina kazi kubwa kwa pointi 20 ilizonazo na mechi nne ilizosaliwa nazo, huku kuanzia Kagera Sugar iliyopo nafasi ya nane yenye pointi 32 hadi ya 14 inayoshikiliwa na KMC yenye pointi 26 kila moja ina nafasi ya kwenda na maji kama hazitazitumia vyema mechi ilizosaliwa nazo kujiokoa.

Mtibwa Sugar ina pointi 29, huku Dodoma Jiji na TZ Prisons kila moja ina 28, Coastal Union na Mbeya City kila moja ina pointi 27 na timu zote zina michezo minne kila moja na hadi Mei 28 lolote linaweza kutokea kwa timu hizo kama hazitajipanga vyema kwani timu mbili zinashuka moja kwa moja na mbili nyingine zanafasi ya 13 na 14 zitacheza play-off zenyewe kwa zenyewe kabla ya kuvaana na mshindi wa Ligi ya Championship zitakazochujanja kwenye hatua kama hiyo.