Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lejendi Al Ahly aipigia hesabu Mamelodi, adai Simba wepesi

Wakati Simba ikifungua michuano ya African Football League Oktoba 20 dhidi ya Al Ahly uwanja wa Mkapa, lejendi wa timu hiyo ya Misri, Mokhtar Mokhtar amesema hesabu zao ni Mamelodi Sundowns.

Mshindi wa mechi ya robo fainali Simba VS Al Ahly ambayo itarudiwa jijini Cairo, Misri atakutana na mshindi wa mechi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini vs Petro de Luanda ya Angola ambapo Mokhtar akizungumza na mtandao wa Kingfut amedai mechi ya Simba itakuwa rahisi kwao.

"Simba ndio wanatakiwa wawaze kuivaa Al Ahly, ila wasiwasi wangu ni kucheza dhidi ya Mamelod kwa maana sisi tunaweza kuifunga timu yoyote Afrika ila mambo yanabadilika tukicheza na Mamelodi," amesema Mokhtar

Timu katika mechi nne zilizopita walizokutana kila timu imeshinda nyumbani (2/2).