Lampard, Mourinho watoleana maneno

Thursday October 01 2020
lampard pic

 London, England. Makocha Jose Mourinho na Frank Lampard wameingia tena katika vuita ya maneno wakati wa mchezo wa Kombe la Carabao uliozikutanisha Tottenham na Chelsea juzi usiku.

Chelsea ilipata bao la kuongoza dakika ya 19, shukrani kwa mkwaju wa Timo Werner, kabla ya Spurs kuswazisha na baadaye kushinda kwa mikwaju ya penalti 5-4.

Dakika tano baada ya bao la Werner, Mourinho na Lampard walilazimika kutenganishwa na mwamuzi wa akiba, Andre Marriner baada ya kuzuka kwa maneno kati ya wawili hao.

Makocha hao, ambao waliwahi kufanya kazi pamoja wakati Lampard akiwa mchezaji wa Chelsea na Mourinho kuwa kocha wake kwa mafanikio, walionekana katika picha za video wakitoleana maneno.

Taarifa kutoka uwanjani zilidai kuwa Mourinho alikuwa akimsema Lampard kuwa alikuwa akiongea sana baada ya timu yake kupata bao la kuongoza.

Kocha huyo wa Spurs, Mourinho, anadaiwa kutoa maneno ya hasira yaliyoambatana na kashfa juu ya Lampard aliyekuwa na maneno zaidi kwa wachezaji wake.

Advertisement

“Ulipopoteza kwa mabao 3-0 haukuwa umesimama hapa kama hivi,” alisema Mourinho katika mbaadhi ya maneno yake akikumbusha jinsi Chelsea ilivyotangulizwa mabao matatu kabla ya kusawazisha dhidi ya West Brom.

 

Advertisement