LaLiga kutazamwa hapa Dar

Wednesday October 20 2021
liga pic
By Leonard Musikula

LaLiga Tanzania leo wameingia makubaliano  na mgawaha wa Samaki Samaki kuwa mgahawa eneo rasmi kutazama mechi zote.

Mwanaspoti limeshuhudia makubaliano hayo ambapo yamewahusisha mwakilishi wa LaLiga Tanzania, Burundi, na Rwanda, Alvaro Payo pamoja na Julius peter ambaye ni meneja matangazo wa mgawaha huo.

Akizungumza na Mwanaspoti Meneja matangazo wa Samaki Samaki amesema wamefurahi ujio wa LaLiga kwao kwani utawapa fursa wateja wao kunufaika zaidi na ushirikiano wao pamoja na Laliga Tanzania.

"Tunawakalibisha Watanzania pamoja na wanamichezo wote kuja kuitazama LaLiga hapa kwetu kwani kuna vitu vingi ambavyo mtanufaika navyo na kutakua na michezo mbalimbali pamoja na zawadi siku ya Jumapili" anasema Julius peter.

Pia mwakilishi wa LaLiga Tanzania naye amesema kua ushirikiano huo utawapa wapenzi wa soka wa hapa nchini kuitazama LaLiga huku wakijua mambo mengi zaidi kuhusiana na Ligi hiyo.

"Lengo la kufanya makubaliano haya ni kuweza kuwafikia wapenzi wa Laliga hapa nchini kupitia mgawaha huu ambapo watu wataweza kuitazama la Liga huku pia wakipata bahati ya kuijua zaidi  LaLiga" amesema Alvaro.

Advertisement
Advertisement