Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa wachezaji hawa Yanga haiwezi kusajili

Muktasari:

Dirisha dogo la usajili kwa wachezaji unategemewa kufungwa Jumamosi hii ikiwa ni mwezi mzima sasa tangu lilipofunguliwa Novemba 15.

Dar es Salaam. Wakati kiungo mchezeshaji wa African Lyon, Haruna Moshi 'Boban' akihusishwa kujiunga na Yanga, miamba hiyo italazimika kupunguza wachezaji kabla ya kusajili katika dirisha hili litakalofungwa Jumamosi.

Yanga inajumla ya wachezaji 29 baada ya Emmanuel Martin kumaliza mkataba wake na kujiunga na Ruvu Shooting na bado inausishwa kusajili baadhi ya nyota dirisha hili la usajili linalotarajiwa kufungwa Desemba 15 mwaka huu.

Miongoni mwa nyota wanahusishwa kutua Yanga ni Boban ambaye hata hivyo taarifa zinasema amejiunga na Kagera Sugar pamoja na Mkongo Ruben Bomba.

Nyota wa Yanga waliopo katika kikosi chao hadi sasa makipa, Klaus kindoki, Benno Kakolanya, Kabwili Ramadhani wakati mabeki ni Abdallah Shaibu 'Ninja' Kelvin yondan, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Gadiel Michael, Andrew vicent na Pato Ngonyani.

Viungo, Papy kabamba, Thaban kamusoko, Jafary Mohammed, Mohammed Issa Banka, Raphael Daud, Pius Buswita, Maka Edward, Feisal Salum 'Fei Toto', Deus Kaseke, Juma Mahadhi, Said Mussa na Said Makapu.

Washambuliaji Matheo Anthony, Mrisho Ngassa, Amis Tambwe, Ibrahim Ajibu, Heriter Makambo, Yusuph Muhilu, na Paul Godfrey.

Pia miongoni mwa nyota waliopo katika kikosi hicho Yohana Nkomola anahusishwa kutolewa kwa mkopo kwenda Namungo timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza wakati Kakolanya akihusishwa kuachwa na Yanga kutokana na kushindikiza kulipwa malimbikizo yake ya mshahara na fedha ya usajili.