Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa beki hii, Mavugo anapitaje?

Laudit Mavugo.

Muktasari:

  • Yanga iliwatuma makocha wake wawili, Juma Mwambusi na Hans Van Pluijm kuisoma Simba ilipocheza mchezo huo wa kirafiki, ila imebainika licha ya kiwango cha juu cha Mavugo hawana presha kwa kuwa safu yao ya ulinzi ni kiboko.

SIMBA wanapiga kelele mitaani baada ya kuona namna straika wao mpya, Laudit Mavugo alivyowapindua kama samaki wachezaji wa AFC Leopards ya Kenya siku chache zilizopita, lakini imebainika kuwa Yanga tayari walishajiandaa na ujio wake na walichokifanya katika safu yao ya ulinzi ni aibu.

Yanga iliwatuma makocha wake wawili, Juma Mwambusi na Hans Van Pluijm kuisoma Simba ilipocheza mchezo huo wa kirafiki, ila imebainika licha ya kiwango cha juu cha Mavugo hawana presha kwa kuwa safu yao ya ulinzi ni kiboko.

Tathmini ya kikosi cha Yanga imebaini kuwa timu hiyo ina mabeki 11 ambao wote ni wa viwango vya juu jambo ambalo pengine linaweza kuwa sumu kwa Mavugo ambaye pamoja na kwamba anaweza kuzitesa timu nyingine za Ligi Kuu, mashabiki wa Simba wangependa kuona anaifunga pia Yanga.

Yanga ilifanya marekebisho kidogo katika safu yake ya ulinzi kwa kuwaongeza mabeki wawili ambao ni Andrew Vincent kutoka Mtibwa Sugar na Hassan Kessy kutoka Simba hivyo kutimiza idadi hiyo ya mabeki 11.

Katika msimu uliopita, Simba na ujanja wao wote ilishindwa kutikisa nyavu za Yanga licha ya Hamis Kiiza kuifungia timu hiyo mabao 19 katika Ligi Kuu. Safu ya ulinzi ya Yanga katika msimu huo iliruhusu mabao 20.

Kwa sasa eneo la beki ya kati kwa Yanga ina watu watano, huku ikiwa pia na kiraka Mbuyu Twite kama tahadhari ya lolote linaloweza kutokea. Mabeki wa kati kwa Yanga ya sasa ni Kelvin Yondani, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Andrew Vincent ‘Dante’ na Pato Ngonyani ambaye pia anamudu kucheza kama kiungo mkabaji.

Katika eneo la pembeni ambalo pia Mavugo anapenda kulitumia kuongeza makali yake kwa Yanga atakabiliwa na ugumu kutokana na uwepo wa mabeki wanne ambao wamekuwa wakijumuishwa katika kikosi cha Taifa Stars.

Kwa upande wa kulia Yanga ina Juma Abdul na Hassan Kessy huku upande wa kushoto wakiwepo Haji Mwinyi na Oscar Joshua.

Kwa ujumla mabeki wa Yanga kwa sasa ni Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Kelvin Yondani, Andrew Vincent, Pato Ngonyani, Hassan Kessy, Oscar Joshua, Mwinyi Haji na Juma Abdul. Mbuyu Twite pia anamudu nafasi ya beki wa kulia na kati.

Chambua anena

Nyota wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua alisema safu ya ulinzi ya Yanga kwa sasa inaonekana kupata watu wa kutosha, huku akidai kuwa beki mpya, Dante tayari ameanza kuonyesha uhai jambo ambalo linaongeza matumaini Jangwani.

“Baada ya Cannavaro na Yondani kucheza kwa muda mrefu kwa pamoja ni dhahiri kuwa tulihitaji kuanza kupata mbadala wao katika nafasi ya beki ya kati, nadhani huyu Andrew ameanza kuonyesha uhai katika nafasi hiyo,” alisema Chambua.

“Kwa sasa Yanga ina safu nzuri ya ulinzi kuna wakati nilidhani wanahitaji mtu mwingine katika eneo hilo kwaajili ya kumwandaa kwa baadaye lakini pia ukiwa na idadi kubwa sana ya mabeki utakuwa unawazibia wengine nafasi,” aliongeza Chambua.