Kundi la Tip Top Connection lasambaratika

Muktasari:
- Kundi hilo linasimamiwa na Meneja wao Babu Tale ambaye pia anamsimamia mwanamuziki Diamond Patnum.
Msanii Tunda Man amesema kundi la Tip Top Connection limesambaratika ambapo kila mtu anafanya kazi kivyake.
Miaka kadhaa inakatika hakuna kazi za pamoja kwa wasanii ambao wanaunda za hilo 'Tip Top Connection' linaloundwa na Dogo Janja, Madee na Tunda Man.
Kundi hilo linasimamiwa na Meneja wao Babu Tale ambaye pia anamsimamia mwanamuziki Diamond Patnum
Tunda aliweka bayana baada ya kuulizwa na MCL Digital akisema, "Daah kitambo kundi limevunjika na ndio maana unaona sasa hivi kila mmoja anatoka kivyake, ila katika maisha ya kawaida tuko pamoja na tunasaidiana mmoja wetu akitoa kazi.
"Na sio haja ya kuendelea kuficha wakati wazi mashabiki zetu wanajua kabisa, sio kawaida yetu kukaa kimya bila ya kutoa kazi mpya katika kundi letu, na wasitegemee kama linaweza kurudi hili kundi."
Tip Top Connection ni kundi lililokuwa maskani yake Manzese, liliwahi kutamba na nyimbo kama, 'Bado tunapanda' 'Riziki' Goma la Manzese na nyingine nyingi.