Kumbe shujaa wa Rashford ni Tim Howard

Muktasari:

  • Rashford, 20, amekuwa tofauti  na wengine baada ya kudai shujaa wake ni kipa, Howard.

STAA wa Manchester United, Marcus Rashford shujaa wake wa utotoni wakati anakuwa ni kipa wa Marekani, Tim Howard.

Wakati mastraika wengi vijana wakifichua kwamba mashujaa wao ni Eric Canton au Ronaldo wa Brazil, fowadi wa England, Rashford, 20, amekuwa tofauti sana baada ya kudai shujaa wake ni kipa, Howard.

Rashford alisema muda wote alikuwa shabiki wa kipa huyo aliyewahi kuichezea Man United kati ya mwaka 2003 na 2006 kabla ya kwenda kudumu kwa muda mrefu sana katika kikosi cha Everton.

Fowadi huyo amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Man United kinachoongozwa na kocha Jose Mourinho.