Kumbe Shikhalo ndiye kamvuta Aucho Yanga
Yanga imshukuru kipa Mkenya ambaye uhakika wataachana naye Faruk Shikhalo anayekubalika na mashabiki wa timu hiyo, Mwanaspoti linafahamu kwamba kiungo wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho alibaki kidogo asisaini Yanga ili atue Simba.
Kiungo huyo kabla ya kufanya maamuzi yoyote aliwasiliana na kipa huyo kisha akataka kujua kama Yanga inalipa wachezaji kwa wakati akiambiwa kwamba timu hiyo hailipi vizuri.
Hata hivyo majibu ya Shikhalo yalimaliza kila kitu akimwambia mpaka wanamaliza mechi ya mwisho hakukuwa na madai yao yoyote na kwamba hawajawahi kucheleweshewa malipo.
Majibu hayo yalimsukuma kiungo huyo kujaa katika 18 za mabosi wa Yanga akiwaambia kwamba anakuja baada ya kujiridhisha,