VIDEO: Aucho amaliza ubishi…. Yanga yaipiga Simba bao la kisigino
YANGA ni kama wataka sifa, kwani kile wanachokifanya kwa sasa ni balaa na wapinzani wao lazima waombe po, ikiwa hata saa 24 hazijatimia tangu imshushe kipa la Mali, Diarra Djigui waliyemtambulisha rasmi jana, wamemleta nyota mwingine mpya Khalid Aucho kininja na kumaliza ubishi uliokuwapo awali juu yake kama atatua Jangwani au Msimbazi.
Mabosi wa Jangwani mwishowe wakaipiga bao Simba kwa kumshusha kiungo huyo mkabaji kutoka Uganda kiWababe hao wa Jangwani ni kama wana kitu wanatengeneza kuelekea msimu ujao, kwa staili yao ya sasa kushusha jembe baada ya jembe, kwani jana ilishusha staa wao wa nne wa kigeni lakini huyu wakimshusha kininja wakiwahofia Simba, iliyokuwa ikitajwa nayo kumvizia.
Kusoma habari hii kwa undani pata Gazeti la Mwanaspoti la Jumatatu Agosti 09, 2021