Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe kina Kelvin, Agiri wapo wengi tu

Dar es Salaam. KOCHA mkuu wa Timu ya Taifa ya Vijana Tanzania chini ya miaka 17 'Serengeti Boys', Oscar Milambo,  amefunguka kwamba katika hatua hii ya kufuzu fainali za Afcon 2017 Kanda ya Cecafa ameficha silaha zake zingine.

Akizungumza na Mwanaspoti, alisema licha ya kuwatumia Agiri Ngoda na Kelvin John katika safu ya ushambuliaji ana washambuliaji wengine ambao wataonekana mwakani.

"Ngoda na Kelvin nimewatumia hapa kwa vile katika mazoezi wameonyesha pacha yao kuwa vizuri, lakini wapo wachezaji wengine ambao nao wana uwezo mkubwa hivyo mwakani wataonekana kabisa na hakutakuwa na tatizo iwapo Ngoda au Kelvin akikosekana," alisemaKocha Mliambo.

Akizungumzia kuhusu wachezaji wake kushangilia mabao kwa staili ya kuomba msamaha, alisema hajajua kwanini wamefanya hivyo lakini inabidi watanzania waelewe kwamba wachezaji wake ni watoto.

"Tangu timu inaanza ujue hatukuwahi kupoteza katika Mashindano yoyote yale, inawezekana hilo jambo liliwaumiza ndio maana, kikubwa tuwe tunawapa moyo vijana kwasababu hawa ni watoto," alisema.

Serengeti ilishika nafasi ya 3 baada ya kuifunga Rwanda kwa penalti 4-3, huku ikifanikiwa kuchukua tuzo ya timu yenye nidhamu na mchezaji bora wa M