Kumbe hiki ndicho kinachowakwamisha wachezaji

Muktasari:
Kile alichokisema Jacob Masawe nahodha wa Gwambina FC kama wachezaji wenzake watakizingatia basi wanaweza wakafikia malengo yao kwa uharaka.
NAHODHA wa Gwambina FC, Jacob Masawe amesema soka bila nidhamu anaamini mchezaji hawezi kufika popote kutokana na matunda yake kuwa wazi.
Masawe amesema kwa uzoefu alionao kwenye soka amebaini sekta hiyo inahitaji nidhamu kubwa ya maisha yao kwa ujumla.
Amesema wachezaji wengi wanajikuta malengo yao yanachukua muda mrefu kutimia kutokana na kushindwa kuishi miiko ya soka.
"Mfano tunatakiwa kupumzika kwa muda mrefu baada ya mazoezi lakini unakuta baadhi yao wanakesha na simu kuchati, anaamka asubuhi kufanya mazoezi kachoka hawezi kufanya kwa asilimia 100,"
"Maisha yetu nje ya soka pia yanapaswa kuwa mfano kutokana na kazi zetu zinatazamwa na watu wengi, hivyo kufanya vitu vya hovyo hovyo ndivyo vinavyofanya heshima yetu kupungua," amesema.