Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuiona Al Merrikh vs Yanga Rwanda kiingilio Sh100,000

KIKOSI cha Yanga kesho kitapaa nchini kuwafuata wapinzani wao nchini Rwanda, El Merreikh ya Sudan kwenye mchezo wa hatua ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika utapigwa Septemba 16 saa 10:00 jioni.

Viingilio katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Pele  ambako El Merreikh wamechagua kuwa Uwanja wao wa nyumbani, vimetangazwa huku kiingilio cha juu kikiwa Sh104,391 ya Tanzania (Franc 50,000), kinachofuatia ni Sh52,195 (Franc 25,000) na cha chini ni Sh20,870 (Franc 10,000).

Yanga ilifuzu hatua hiyo kwa ushindi wa jumla ya mabao 7-1, baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kushinda 2-0.


El Merreikh ilifuzu kwenda hatua ya kwanza ya mtoano kwa faida ya bao la ugenini baada ya kulazimishwa suluhu hiyo ya bila kufungana ambapo awali walitoka sare ya bao1-1 dhidi ya Otoho d'oyo ya Congo Brazzaville.